Wizara ya maendeleo ya Jamii jinsia Wananwake na makundi maalum imeitaka jamii kutumia fursa na rasilimali zilizopo katika maeneo yao ili kuleta maendeleo endelevu kwa familia, jamii na Taifa kwa ujumla pamoja na kuhakikisha hawanzishi Migogoro katika maeneo yao.
Wito huo umetolewa na Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Amon Mpanju katika uzinduzi wa Kampeni ya Amsha Ari yenye lengo la kuleta mageuzi ya kifikra na mtazamo ili kuwafanya Wananchi kujua umuhimu wa kushiriki katika maendeleo.
Pamoja na mambo mengine Wakili Amon ameitaka jamii kuacha kuanzisha Migogoro badala yake kuhakikisha wanajikita kufuta Migogoro hiyo ilikuounguza safari za Mahakamani zisizo kuwa na tija lakini pia amewataka pindi wanapopeleka kesho wajitahidi kuhakikisha wanatoa ushirikiano wanapohitajika.
Tujikite kwenye kuwekeza kuzuia Migogoro Mahakama hatutaiona ila inapotokea shauri limepelekwa Mahakamani semeni ukweli kama mtu amefanya makosa”Alisema Amon Mpanju Naibu Katibu Mkuu Maendeleo ya jamii jinsia na makundi Maalum.