Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt Selemani Jafo ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Kisarawe ameiagiza ofisi ya Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe kujenga Zahanati Maalum yenye muuguzi katika Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Jokate Mwegelo ili kuwapa wanafunzi huduma muhimu za Afya kwa haraka.
Maagizo hayo yametolewa na Waziri Jafo baada ya kupokea ombi kutoka kwa wanafunzi kusogezewa huduma za Afya Shuleni hapo ambapo kwa sasa ina zaidi ya wanafunzi 1700 wa kidato cha kwanza hadi sita wanaotegemea zahanati ya Kijiji cha Mhaga hali inayopelekea zahanati hyo kulemewa kutoa huduma kwa wanakijiji na wanafunzi hao
“Tuna watoto Elfu moja plus, hawa watoto ni wengi mwambie Mkurugenzi tuanze mchakato wa kutenga chumba maalumu iwe kama zahanati ya shule na kuhakikisha anamleta mtaalamu wa afya hapa anaanza kutoa huduma ya afya hapahapa shuleni, yale matatizo makubwa zaidi yataende huko mbele lakini huduma za msingi kabisa tuweze kuwasaidia vijana wetu hawa hapahapa, watoto wa kike wanataka huduma ya karibu”.
Changamoto zingine zilizowasilisha na Mkuu wa Shule hiyo Mariamu Mpunga ni pamoja na Uhaba wa mahabara na vifaa vya majaribio ya kisayansi kulinganisha na hikama ya wanafunzi wa michepuo ya sayansi “Shule yetu ina sayansi piwa sometimes inatupepelekea kurudi nyuma kutokuwa imara inavyotakiwa”.
Sambamba na hayo Mwalimu Mpunga ameeleza shule inakabiliwa na ukosefu wa nyumba za walimu ikilinganisha shule ipo kijijini mahali pasipo kuwa na nyumba nzuri za kupangisha. Amesema kwa sasa shule ina nyumba mbili tu za Walimu hali inayotatiza jitihada wanazofanya za kuendesha vipindi vya ziada usiku na mwishoni mwa juma kwa walimu wengi hulazimika kuondoka mapema kwa kukosa makazi ya karibu na shule.
Akijibu maombi hayo Dkt Jafo amesema Serikali imetenga Tsh. Milioni 95 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za walimu, “ninafahamu walimu wetu wanachangamoto za nyumba, tulihangaika tukapata nyumba chache za kuanza takribani 2. Niwahakikishie Serikali tumepata milioni 95 kwa ajili ya kujenga nyumba ya walimu two in one kwanza kwa kuanzia ambao ujenzi huu utaanza hapa katikati muda si mrefu sana”
Aidha amesema wanatazamia kuanza ujenzi wa maabara mpya shuleni hapo kabla ya mwaka 2025 haujaisha ili kukidhi hikama kubwa ya wanafunzi wanaosoma michupuo ya sayansi.
Dkt. Jafo ameahidi kufanya shule ya Sekondari ya wasichaba ya Jokate mwegelo kuwa ya bora ya mfano ngazi ya Taifa.
Shule ya Sekondari ya Wasichana iliyopo Wilayani kisarawe Kata ya Kibuta Kijiji cha Mhaga ilianzishwa ilifunguliwa rasmi mnamo mwaka 2021 chini ya vuguvugu la TOKOMEZA ZIRO kampeni iliyoasisiwa na aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe kwa wakati huo, Jokate Mwegelo kwa lengo la kuongeza ufaulu miongoni mwa watoto wa kike kwa kufuta daraja Ziro ambapo Mpaka sasa imeshatoa wahitimu wa kidato cha sita awamu 2, kidato cha nne awamu moja huku ikifanya vizuri katika matokea ya mitihani hiyo kwa kupata ufaulu wa asilimia mia moja.