Latest Posts

“JUKUMU LA KUWALEA WENYE MAHITAJI SI LA WENYE VITUO PEKEE” DC SHAKA

Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Shaka Hamdu Shaka amewaasa walezi wa vituo vya kulelea watoto wenye mahitaji maalum kuwalea watoto hao katika maadili mema ili kuliandaa Taifa bora la kesho

Shaka amesema hayo wakati akikabidhi zawadi za Eid El- fitr akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Adam Malima zilizotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ambapo amesisitiza kuwa maadili ndio nguzo kuu ya uwepo wa amani na utulivu hapa Nchini.

Aidha, Shaka amesama kuwa jamii itambue kuwa jukumu la kuwalea watoto yatima na wenye mahitaji maalum si la wenye vituo pekee au la Serikali bali ni la jamii nzima.

Kaimu Afisa Ustawi wa Jamii Mkoa wa Morogoro Hamisa Kagambo amesema kuwa kama Mkoa wataendelea kumpongeza Rais Samia pia wataendelea kuwakumbuka wenye uhitaji

Kwa upande wake Shekhe wa Wilaya ya Kilosa Nasoro Mirambo amemshukuru Rais Samia kwa kuwakumbuka wenye uhitaji kwani amesema kufanya hivyo ni faraja kwa watoto hao, huku baadhi ya walezi wa watoto waliopata zawadi hizo wameiomba jamii iendelee kuwakumbuka watoto hao wenye uhitaji.

Zaidi ya watoto 300 vituo 5 vya kulea watoto pamoja na kituo cha kurekebisha tabia (Magereza) Wilaya ya Kilosa wameguswa na mkono wa Eid wa Rais Samia ndani ya Mkoa wa Morogoro .

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!