Na Helena Magabe -Tarime
Kampeni ya Amsha Ari yenye lengo la kuleta mageuzi ya kifikra na mtazamo ili kuwafanya Wananchi kujua umuhimu wa kushiriki katika maendeleo kupitia Wizara ya Katiba na Sheria kwa kushirikiana na Wizara ya maendeleo ya mezinduliwa rasmi Wilayani Tarime Mkoani Mara na kisha kutekelezwa katika mikoa 26 nchini.
Kampeni hiyo ya mageuzi ya Kifikra na mtazamo kwa Jamii kuwa kitovu cha maendeleo yenye kauli mbiu isemayo “SAMIA NA MAENDELEO MPAKA KIELEWEKE” imezinduliwa leo Aprili 13, 2925 imeshirikisha Halmaahauri zote mbili za Wilaya ya Tarime Viongozi wa Serikali ngazi ya Mkoa na Wilaya,Tasisi mbali mbali za Serikali na binafsi ,Viongozi wa Dini,Viongozi wa Kisiasa pamoja na makundi maalumu pamoja na wakuu wa idara mbali mbali lengo lake ni kushirikisha Jamii yote katika maendeleo endelevu na jumuishi.
Akizindua mafunzo hayo Naibu katibu Mkuu maendeleo ya Jamii na makundi maalumu Wakili Amon Mpanju amesema kampeni hiyo ni mahususi kwaajiri ya kubadirisha fikra ,mtazamo na mawazo ya Wananchi ili wawe chachu na kitovu cha maendeleo ndani ya Jamii wanamoishi.
” Hatutaacha kufika katika kata yoyote ndani ya Wilaya ya Tarime yenu ya Tarime kwa kuwa Dokta Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Serikali anayoingoza anaamini kuwa Jamii ikishirikishwa katika swala hili kutakuwa na maendeleo endelevu na jumuishi” amesema ” Naibu Mpanju
Wakili wa Serikali Zacharia Mzese amesema wamefanikiwa kufanya kampeni ya msaada wa kisheria lengo ni kutoa msaada wa kisheria kwa Watu ambao hawana uwezo wa kumudu ghalama za Mawakili ambapo Disemba 2024 walifika Tarime na kutoa elimu kwa Halmashauri zote mbili na kufanikiwa kuwafikia Wananchi 18,000.
Migogoro ilikuwa 133 ipo waliyotatua wakati wa kampeni lakini mingine ilikuwa ikiendelea kushughulikiwa na ngazi ya Kiutawala vile vile walibaini migogoro yenye maslahi mapana mfano katika Halmaahauri ya Tarime Mji walibaini mgogoro wa soko la Rebu na kwa upande wa Halmashauri ya Tarime Vijiji walibaini mgogoro wa maswala ya shule katika Kijiji cha Kubori ,mgogoro katika Kijiji Cha Tagare na Kenyamsabi.
“Kiongozi wetu wa Katiba na Sheria Eliakimu Maswi ametuelekeza tusikilize na kutatua migogoro hii lakinj pia tuungane na Wizara ya maendeleo ya Jamii na na Tamisemi kwaajili ya uzinduzi wa kampeni hii” alisema Wakili Mzese
Mwenekiti Baraza la ushauri la Wazee Mkoa wa Mara Mzee Joseph Nyairaha aliomba ufafanuzi ni kwanini kundi la Wazee halipo kwenye makundi mengine ,kwanini maswala yao yanawekwa kando hata wakiomba mikopo hawapati licha ya kuwa Wana uwezo wa kuzalisha na kukuza uchumi lakini sera ya Wazee ina miaka 25 lakini haitungiwi sheria.
Bonny Matto Mkurugenzi wa haki za Binadamu Shirika la Tuwakomboe Paraligo alisema Wilaya ina Maafisa ustawi wawili tu Mmoja Tarime DC na Mwingine Tarime TC lakini Wizara yamaendeleo ya Jamii imeajiri watumishi 1800 na kupendekeza kuwa kama Serikali haiwezi kuajiri maafisa ustawi wa Jamii ni vema Maafisa maendeleo wakasaidia na kazi za ustawi wa jamii na kuongeza kuwa Wazee wazee wakulima ambao wamelima miaka 65 na kukuza uchumi kwenye Nchi walipwe pensheni.