Latest Posts

Eneo maalumu la makubaliano ya uwekezaji wa wanyamapori (SWICA) ni eneo lililotengwa ndani ya hifadhi ya wanyamapori au pori la akiba ambapo mashirika au watu binafsi hupewa haki ya kuwekeza katika shughuli zinazohusiana na wanyamapori kama vile utalii.

“Eneo maalumu la makubaliano ya uwekezaji wa wanyamapori (SWICA) ni eneo lililotengwa ndani ya hifadhi ya wanyamapori au pori la akiba ambapo mashirika au watu binafsi hupewa haki ya kuwekeza katika shughuli zinazohusiana na wanyamapori kama vile utalii, uwindaji au uhifadhi, maeneo haya maalumu yalianzishwa ili kukuza usimamizi endelevu wa wanyamapori, kupata mapato kwa ajili ya juhudi za uhifadhi, kuchochea maendeleo ya kiuchumi katika maeneo ya vijijini, na kuhakikisha ulinzi wa viumbe hai na makazi asilia” -Kichere “Kwa mujibu wa kanuni ya 3(1) ya kanuni za eneo maalumu la uwekezaji kwa wanyamapori za mwaka 2020 Waziri wa Maliasili na Utalii amepewa mamlaka baada ya kupata mapendekezo ya bodi ya mamlaka ya usimamizi wa wanyamapori Tanzania (TAWA) kuteua maeneo ya ardhi ndani ya mapori ya akiba kuwa maeneo maalumu ya makubaliano ya uwekezaji wa wanyamapori kwa madhumuni yaliyoainishwa katika kanuni hizi” -Kichere “Hata hivyo, mamlaka ya usimamizi wa wanyamapori Tanzania (TAWA) ilitoa hati za ugawaji wa maeneo ya uwindaji (vyeti namba TAWA.0003, TAWA.0004 na TAWA.0005) kupitia makubaliano ya eneo maalumu la uwekezaji kwa wanyamapori kwa wawekezaji wawili kwenye jumla ya maeneo 13, ingawa maeneo hayo hayakupata idhini ya Waziri kuwa vitalu vya uwindaji kama inavyotakiwa kisheria, hali hii inaonesha kuwa menejimenti ya mamlaka ya usimamizi wa wanyamapori Tanzania haikuzingatia majukumu ya Waziri wa Maliasili na Utalii kabla ya kutoa hati husika” -Kichere “Ni maoni yangu kuwa kutoa hati hizo kwa maeneo ambayo hayajapata idhini ya Waziri ni kukiuka kwa kiasi kikubwa kanuni za sneo maalumu la makubaliano ya uwekezaji wa wanyamapori za mwaka 2020 na kuleta shaka kuhusu uwazi na uadilifu wa mchakato wa ugawaji wa maeneo hayo, napendekeza serikali ihakikishe TAWA inazuia ugawaji wa maeneo maalumu ya uwekezaji kwa wanyamapori bila idhini ya Waziri” -Kichere CAG Charles Kichere amezungumza hayo alipokutana na wanahabari Aprili 15.2024

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!