
Katibu wa CCM Mkoa wa Iringa, Said Goha, akiambatana na wajumbe wa Sekretarieti ya CCM Mkoa wa Iringa, wamefurahishwa na ushirikiano mzuri wa viongozi wa Wilaya ya Iringa Vijijini na kuwasihi waendelee kudumisha umoja na upendo katika kipindi hiki cha uchaguzi mkuu.
Akizungumza leo na viongozi wa kata na matawi katika kata nne za Wilaya ya Iringa Vijijini, Katibu wa CCM Goha amewasihi viongozi hao kufanya siasa nzuri na kuepuka kuingia katika makundi ambayo hayana tija. Alisisitiza kwamba kipindi hiki cha uchaguzi bado kinahitaji utulivu kwani viongozi wengi bado wapo madarakani.
“Wilaya yenu imetulia, hivyo niwaombe viongozi, tuendelee kufanya ziara mbalimbali za kazi ili kuzungumzia miradi ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais wetu, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambaye ameleta miradi mikubwa ya kimkakati katika kata zenu,” alisema Goha.