Katibu wa CCM Wilaya ya Iringa Vijijini, Ndg. Sure Mwasanguti, leo amefika katika Kituo cha Kuandikisha Wapiga Kura wa Serikali za Mitaa kilichopo Ofisi ya Kijiji cha Kalenga, mkoani Iringa, na kujiandikisha kwenye Daftari la Wakazi, tayari kushiriki uchaguzi utakaofanyika tarehe 27 Novemba, 2024.
Akizungumza baada ya kukamilisha utaratibu huo, Katibu Mwasanguti amewahimiza wananchi wote kujitokeza kujiandikisha katika daftari hilo la wakazi kuanzia Oktoba 11 hadi 20, 2024.