Katibu wa JuimuiUmoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Wilaya ya Iringa Vijijini, Bi. Sophia Nyalusi, leo Aprili 14 ameadhimisha siku yake ya kuzaliwa kwa namna ya kipekee kwa kutembelea na kutoa msaada katika makundi maalumu.
Katika maadhimisho hayo, Katibu Sophia ametembelea Madrasa ya Kalenga ambapo alitoa Juzuu 50 kwa wanafunzi pamoja na kushiriki nao vinywaji na kuwapatia mahitaji mengine muhimu.
Aidha, hakuishia hapo, kwani aliendelea kwa kuwatembelea watoto wenye mahitaji maalum na kuwapatia chakula kama njia ya kuwafariji na kuwaunga mkono katika maisha yao ya kila siku.
Wananchi walioshuhudia tukio hilo wamesema kuwa hatua hiyo ni ya kuigwa na inaonesha moyo wa huruma na uwajibikaji wa viongozi kwa jamii, hususan kwa makundi yanayohitaji msaada wa karibu.