Jumla ya Kaya 41,709 zilipo katika vijiji na mitaa 60 ambapo ni makundi maalum kupitia TASAF Mkoani Kilimanjaro zimetambuliwa na uandikishwaji unaendekea ili kupatiwa huduma ya bima ya afya kwa wote
Hayo yameelezwa Februari 24,2026 na Katibu wa Siasa, Itikadi na uenezi wa Ccm Mkoa wa Kilimanjaro Komredi Abraham Urio wakati alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari juu ya yaliyotekelezwa katika siku mia Moja za Rais Dkt.Samia Hassan.
Amesema kuwa katika siku mia moja Mkoa wa Kilimanjaro umepokea kiasi cha shilingi Bilioni 112.63 za miradi ya maendeleo ikiwemo mradi wa stendi ya Mabasi Ngangamfumuni,stendi ya mabasi Mwanga,ujenzi soko la Kwasadala,ujenzi wa bwawa la maji la Yongoma Wilayani Same pamoja na fedha za miradi wa umeme katika baadhi ya vitongeji vilivyokuwa bado havijafikiwa na huduma hiyo.