Latest Posts

KIONGOZI WA UPINZANI MISRI, AL-TANTAWI AACHIWA HURU BAADA YA KIFUNGO CHA MWAKA MMOJA

Kiongozi maarufu wa upinzani nchini Misri, Ahmed al-Tantawi, ameachiwa huru baada ya kutumikia kifungo cha mwaka mmoja gerezani kwa tuhuma za kukiuka sheria za uchaguzi. Taarifa ya kuachiliwa kwake imetangazwa na wakili wake, Khaled Ali, kupitia mtandao wa kijamii X (zamani Twitter).

Al-Tantawi, ambaye alionekana kuwa mpinzani wa kweli pekee dhidi ya Rais Abdel Fattah al-Sissi katika uchaguzi wa mwaka 2023, alijikuta nje ya kinyang’anyiro hicho baada ya kushindwa kupata idadi ya sahihi zinazohitajika kuidhinisha kugombea urais. Alilalamika hadharani kuwa serikali na watu waliomtii Al-Sissi walikwamisha harakati za waungaji mkono wake, hatua iliyochukuliwa kama njia ya kumwekea vizingiti kisiasa.

Mnamo Februari 2024, al-Tantawi na wasaidizi wake 22 wakiwemo wakurugenzi wa kampeni walihukumiwa kifungo cha mwaka mmoja jela kwa kusambaza fomu zisizotambuliwa rasmi za uidhinishaji wa kugombea urais, jambo ambalo lilihesabiwa kuwa kinyume cha sheria za uchaguzi za nchi hiyo.

Tangu Rais Abdel Fattah al-Sissi aingie madarakani mwaka 2014, baada ya jeshi kumuondoa aliyekuwa rais wa kwanza kuchaguliwa kidemokrasia, Mohammed Mursi, serikali yake imekuwa ikishutumiwa kwa kukandamiza wapinzani wa kisiasa na uhuru wa kisiasa nchini humo.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!