Tarehe 10 Machi, 2025
Picha za matukio mbalimbali katika Kongamano la Wanawake na Uongozi Katika Elimu lililofanyika kama sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani (International Women’s Day) lililoandaliwa na ADEM kwa kushirikiana na programu ya SHULE BORA lililolenga kuangazia mchango wa wanawake katika uongozi kwenye sekta ya elimu.
Maadhimisho hayo yamefanyika leo tarehe 10 Machi, 2025 jijini Dar es Salaam ambapo Walimu wanawake kutoka ngazi mbalimbali wamekutana kusikiliza mijadala, hotuba za hamasa, na mafunzo kutoka kwa viongozi waliotangulia.
Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu (ADEM) na SHULE BORA zinashirikiana katika utoaji wa mafunzo kuhusu uongozi na usimamizi wa elimu kupitia uanzishwaji wa Jumuiya za kujifunza kwa Walimu Wakuu na Maafisa Elimu Kata ambapo kupitia mafunzo hayo iligundulika kuwa asimia 15 tu ya viongozi hao waliopatiwa mafunzo ni wanawake huku asilimia 85 wakiwa ni wanaume hivyo takwimu hizo zimepelekea kufanyika kwa kongamano hilo ili kuhamasisha wanawake katika sekta ya elimu nchini kuzifuata fursa za uongozi kwa kutumia njia mbali mbali iliwa ni pamoja na kuhudhuria mafunzo ya Uongozi na Usimamizi wa Elimu yanayotolewa na ADEM.
Programu ya SHULE BORA inatekelezwa katika Mikoa tisa ya Tanzania Bara ambayo ni Dar es Salaam, Pwani, Tanga, Dodoma, Singida, Kigoma, Katavi, Simiyu na Shinyanga.
Kongamano hilo limehudhuriwa na viongozi mbalimbali kutoka Ofisi ya Raisi Utumishi, Maafisa Elimu wa Mikoa na Wilaya, ADEM, SHULE BORA, Walimu Wakuu, Ubalozi wa Uingereza, CAMFED, Tume ya Utumishi wa Walimu, Chuo Kikuu Dar es Salaam na Chuo Kikuu cha Tumaini.