Latest Posts

KOREA KASKAZINI YARUSHA MAKOMBORA SAA CHACHE BAADA YA MAZOEZI YA KIJESHI YA MAREKANI NA KOREA KUSINI

Korea Kaskazini imerusha makombora kadhaa ya masafa marefu baharini Jumatatu, ikiwa ni saa chache baada ya wanajeshi wa Korea Kusini na Marekani kuanza mazoezi yao ya pamoja ya kila mwaka, hatua ambayo Pyongyang imekuwa ikiitafsiri kama majaribio ya uvamizi.

Kwa mujibu wa Jeshi la Korea Kusini, makombora hayo yaligunduliwa yakirushwa kutoka jimbo la Hwanghae, ingawa haijafahamika umbali wake wala madhara yaliyosababishwa. Tukio hili ni jaribio la tano la kurusha makombora mwaka huu kutoka Korea Kaskazini, jambo linaloibua wasiwasi juu ya ongezeko la mivutano ya kijeshi katika Rasi ya Korea.

Mapema Jumatatu, wanajeshi wa Korea Kusini na Marekani walianza mazoezi yao ya kijeshi ya pamoja ya siku 11 yajulikanayo kama Freedom Shield, huku wakisitisha kwa muda mafunzo ya moja kwa moja ya ufyatuaji risasi. Hatua hiyo ya kusitisha ufyatuaji wa risasi inakuja baada ya ndege mbili za kivita za Korea Kusini kushambulia kimakosa eneo la raia wakati wa mazoezi ya kijeshi wiki iliyopita.

Taarifa rasmi ya serikali ya Korea Kaskazini imeeleza kuwa mazoezi hayo ni “kitendo hatari cha uchochezi” ambacho kinaongeza uwezekano wa kuzuka kwa vita vya kijeshi katika rasi hiyo.

Mazoezi ya pamoja kati ya Marekani na Korea Kusini yamekuwa yakizua malalamiko makali kutoka Pyongyang, ambayo mara kwa mara hujibu kwa kufanya majaribio ya makombora, ikiwa ni njia ya kuonesha upinzani wake dhidi ya kile inachokiita tishio kwa usalama wake wa kitaifa.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!