Latest Posts

KUELEKEA UCHAGUZI MKUU WAGANGA WA TIBA ASILI WAASWA KUEPUKA IMANI ZA KISHIRIKINA

Na Theophilida Felician.

Waganga wa tiba asili na tiba mbadala nchini wametakiwa kuwa makini na kuepuka kushiriki imani za kushirikina ili kuepukana na madhara yanaweza kusababishwa na imani hizo kwa jamii.

Hayo yamebainishwa na katibu mkuu wa chama cha waganga TAMESOT  Bw Lukas Joseph Mlipu katika taarifa yake aliyoitoa baada yakuhitimisha maadhimisho ya wiki ya tiba asili ya mwafrika yaliyokuwa yakifanyika mkoani Dodoma tangu Tarehe 25  na kuhitimishwa Tarehe 31 Agost  mwaka huu wa 2025.

Katibu Lukas amesema maadhimisho hayo yamewakutanisha waganga kutoka mikoa mbalimbali ambapo dhamira  ya kuwakutanisha pamoja ni kuwapa elimu stahiki yenye kuwaongezea ujuzi na maarifa katika utoaji huduma yatiba kwa wananchi, kuzingatia miongozo muhimu na misingi ya tiba asili kutoka baraza la tiba asili na tiba mbadala namengineyo mengi.

Amesema katika  maadhimisho hayo zilitolewa nasaha mbalimbali  kwa waganga zikiwataka kuyaepuka mambo yanayokwenda kinyume na miongozo ya taaluma ya tiba asili  hasa ramuli chonganishi na imani za kishirikina  hususani  kipindi hiki muhimu  cha uchaguzi mkuu wa madiwani, wabunge na Rais kwani imani hizo zinaweza kuchochea hali ya uvunjifu wa amani kwa jamii husika.

Kiongozi huyo  ameeleza kuwa maadhimisho ya tiba asili ya mwafrika kwa mwaka huu haya kufanikiwa vizuri kutokana na uchache wa waganga waliojitokeza kushiriki akizibainisha baadhi ya sababu zilizopelekea hali hiyo ni mwamuko mdogo uliokuwepo  kwa baadhi ya  waratibu wa wabaraza la tiba asili  mikoa na wilaya katika zoezi la  kuwahamasisha  ushiriki maadhimisho hayo.

Hata hivyo amewashukuru waganga wote waliojitokeza na kushiriki vyema tukio hilo  mwaka huu ambapo  amewasihi  kuyazingatia yote waliyonufaika nayo  kwenye  matukio ya wiki hiyo  huku akiishukuru serikali ilivyokuwa nao bega kwa bega hadi kukamilisha shughuli za wiki ya tiba  asili ya mwafrika  bila kuvisahau vyama vingine vya waganga vilivyoshirikiana na TAMESOT katika zoezi zima la tamasha.

Katibu mkuu  huyo ambaye aliifikia mikoa 11 ya Tanzania bara  alikuwa miongoni mwa wa jumbe 15 walioteuliwa kuwafikia waganga na kuwahamasisha juu ya kufahamu umuhimu wa wiki yatiba asili ya mwafrika  kwa waganga nchini.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!