Latest Posts

MA DC, MA RC WAPEWA RUNGU KUPAMBANA NA CHOKOCHOKO

 

Na Josea Sinkala, Mbeya

Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Serikali za mitaa (TAMISEMI) Mhe. Mohammed O. Mchengerwa, amewaagiza wakuu wa wilaya na mikoa nchini kuhakikisha wanapambana na watu au vikundi vya watu watakaojaribu kuhatarisha amani katika jamii.

Waziri Mchengerwa ametoa agizo hilo wakati akizungumza na wananchi wa jimbo la Mbeya vijijini na viongozi mbalimbali katika shule ya sekondari Lwanjilo wilayani Mbeya kwenye uwekaji jiwe la msingi vyumba vinne vya madarasa na mabweni mawili katika shule hiyo kwa ajili ya kidato cha tano na sita.

Amewataka wananchi kuendelea kufanya kazi kwa bidii kwa maendeleo yao na Taifa kwa ujumla akisema Serikali iko pamoja nao na kwamba ndio maana inaendelea kuwapelekea miradi katika sekta mbalimbali ikiwemo barabara, elimu na afya hivyo wasisikilize maneno ya watu wasiolitakia mema Taifa akidai wametumwa na vibaraka wao (bila kuwataja).

“Mimi niwasihi (Wananchi), nyie endeleeni kufanya kazi mpate mazao wenye kuuza wauze, hatutakubali kuona watu wachache wanatumiwa na vibaraka wao kuliharibu Taifa hili. Na niwatake wakuu wa wilaya shughulikeni na watu watakaojaribu kuleta chokochoko, haya ndio maelekezo yangu kwa wakuu wa wilaya na mikoa nchi nzima”, ameeleza Waziri wa TAMISEMI Mhe. Mohammed Mchengerwa.

Waziri wa TAMISEMI Mhe. Mohammed Mchengerwa, amefanya ziara ya siku moja mkoani Mbeya ambapo ametembelea na Halmashauri tatu za jiji la Mbeya, Halmashauri ya wilaya ya Mbeya na Chunya ambako amezindua na kuweka mawe ya msingi miradi mbalimbali ya maendeleo na kuzungumza na wananchi.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!