Latest Posts

MAAMBUKIZI YA MALARIA KAGERA YAPUNGUA KATIKA KIPINDI CHA JANUARI-MACHI, 2025

 

Theophilida Felician.

Kiwango cha maambukizi ya Malaria kwa mkoa Kagera kimepungua kutoka 34.9% mpaka 29.4% kwa kipindi cha mwezi januari hadi machi mwaka huu wa 2025 licha ya maambukizi kupanda kwa Ngara, Biharamulo na Kyerwa.

Akisema hayo mratibu wa Malaria mkoa Kagera katika hospitali ya rufaa Bukoba Dr Carlos Christian amesema kuwa jitihada mbalimbali zimekuwa zikifanyika katika mapambano dhidi yakuutokomeza ugonjwa huo.

Amefafanua kwamba kiwango cha maambukizi zaidi ni kwa watoto walio chini ya umri wa miaka 5 ukilinganisha na makundi mengine ambapo mambukizi kwa wilaya ya Ngara yanaongoza kwa 51.5% Biharamulo 36.6% Kyerwa 34.9% na Bukoba DC 29.6%.

Aidha amezitaja jitihada zilizopelekea kupungua kwa maambukizi nipamoja na kutoa elimu ya kujikinga na maleria kupitia njia tofautitofauti ikiwemo ya wahudumu wa afya ngazi ya jamii, vyombo vya habari kupewa dawa kinga wananchi, vyandarua na mengineyo.

Ameongeza kwamba hata vifo vitokanavyo na ugonjwa huo vimepungua ukilinganisha na mwaka jana wa 2024.

Amesisitiza kuwa mapambano dhidi Malaria ni ya watu wote hivyo wananchi yawapasa kuendelea kuzingatia maelekezo ya watalaamu ili kujikinga na maambukizi huku akiwahimiza kuwahi vituo vya kutolea huduma ya afya wanapohisi kuwa na dalili za Malaria.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!