Latest Posts

MAKALLA KUANZA ZIARA MKOANI MTWARA APRILI 14, 2025

 

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) wa Itikadi,Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi CCM CPA Amos Makalla anatarajia kuanza ziara ya kikazi mkoani Mtwara kuanzia Aprili 14 hadi Aprili 18,2025.

Taarifa hiyo imetolewa leo Aprili 12,2025 na Katibu wa Siasa,Uenezi na Mafunzo CCM mkoa wa Mtwara Juma Namkoveka kuwa Makalla atatembelea wilaya tano zilizopo mkoani humo.

Aidha wilaya hizo tano zinazotarajiwa kutembelewa na Katibu huyo wa NEC ikiwemo wilaya ya Mtwara,Tandahimba,Newala,Masasi na Nanyumbu.

Aidha ziara hiyo inalenga kuhimiza uimarishaji wa itikadi,maadili ya chama hicho pamoja na kufanya ufuatiliaji na utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya chama hicho ya mwaka 2020,2025 kisha kusikiliza changamoto za wanachama na wananchi kwa ujumla.

 

Hata hivyo Namkoveka amewaomba wananchi mkoani humo kujitokeza kwa wingi katika mikutano itakayofanyika kwenye wilaya hizo na kutoa ushirikiano wa kutosha kwa Katibu wa NEC.

Kwa upande wao baadhi ya wanachama wa chama hicho wamesema wanaimani kuwa ziara hiyo itazidi kuimarisha chama na wako tayari kupokea maelekezo ya kiongozi kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!