Waziri Mkuu wa zamani wa Mali, Moussa Mara, amefunguliwa mashtaka ya “kudhoofisha uhalali wa mamlaka ya dola” kufuatia chapisho aliloweka katika mtandao wa kijamii wa X (zamani Twitter) kuhusu ziara yake kwa wafungwa wa kisiasa.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mwendesha mashtaka wa wa mji wa Bamako Ijumaa, Mara ambaye alihudumu kama Waziri Mkuu kwa kipindi kifupi kati ya mwaka 2014 na 2015 alifikishwa mahakamani kwa kosa linalohusiana na maudhui ya chapisho lake la tarehe 4 Julai 2025, ambako alizungumzia kuhusu kuwatembelea wafungwa wa kisiasa na kuahidi kufuatilia haki zao.
Taarifa iliyochapishwa na Citizen Digital, Moussa Mara anasalia rumande akisubiri kesi yake kusikilizwa Septemba 29, kwa mujibu wa mamlaka za mahakama.
Wakili wake amelaani hatua hiyo, akitaja kuwa ni kuingilia uhuru wa kujieleza na haki ya kidemokrasia ya kutoa maoni.