Latest Posts

MAMLAKA YA RSF YASAMBARATIKA: KAMANDA AJIUNGA NA JESHI LA SUDAN

Jeshi la Sudan limetangaza siku ya Jumapili kuwa kamanda mmoja kutoka kwa wapinzani wao, vikosi vya wanamgambo wa RSF, amejiengua akiwa na baadhi ya wanajeshi wake, hatua ambayo inaweza kuwa ya kwanza kufanywa na kiongozi wa juu tangu pande hizo mbili zianze kupigana zaidi ya miezi 18 iliyopita.

Hakukuwa na tamko lolote kutoka kwa RSF, ambao wamechukua udhibiti wa sehemu kubwa ya nchi katika mgogoro na jeshi ambao Umoja wa Mataifa unasema umesababisha moja ya migogoro mikubwa ya kibinadamu duniani.

Wafuasi wa jeshi walipakia picha mitandaoni wakidai kuwaonesha Abuagla Keikal, afisa wa zamani wa jeshi ambaye alikuja kuwa kamanda mkuu wa RSF katika jimbo la kusini mashariki la El Gezira baada ya kujiengua.

Jeshi, ambalo hivi karibuni limeripoti mafanikio dhidi ya RSF katika baadhi ya sehemu za mji mkuu, lilisema Keikal aliamua kujiengua kutokana na “ajenda mbaya” ya kikosi chake cha zamani.

Halikuweka maelezo zaidi na hakukuwa na taarifa yoyote, iwe kwa maandishi au video, kutoka kwa Keikal.

Mgogoro huo umehamisha zaidi ya watu milioni 10, na kuisukuma sehemu ya nchi hiyo kwenye njaa kali au ukame, huku ukivuta mataifa ya kigeni ambayo yameyasaidia pande zote mbili kwa msaada wa vifaa.

Jeshi na RSF hapo awali walikuwa wakishirikiana madaraka baada ya kufanya mapinduzi mwaka 2021, miaka miwili baada ya kiongozi wa muda mrefu, Omar al-Bashir, kupinduliwa katika uasi wa wananchi.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!