Latest Posts

MAPINDUZI YA TIBA UTALII: HOSPITALI YA RUFAA MBEYA YAUNGANA NA AGA KHAN KUVUTIA WAGONJWA WA NCHI JIRANI.

Ikiwa ni jitihada za kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi, Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya kwa Kushirikiana na Hospitali ya Aga Khan Tanzania zimesaini makubaliano ya kushirikiana katika utoaji wa huduma mbalimbali kwa wananchi.

Akizungumza baada ya kusaini makubaliano hayo Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya Dkt. Godlove Mbwanji amesema, lengo kubwa la makubaliano hayo ni kushirikiana katika maeneo mbalimbali ya utoaji wa huduma kwa wananchi  pamoja na kuendelea kujengeana uwezo mbalimbali wa kitaalamu katika maeneo  utoaji wa huduma za afya kwa jamii.

“…lengo kubwa la kikao cha ni kusaini makubalino ambayo yanaziwezesha hizi taasisi mbili kushirikiana katika maeneo mbalimbali katika kuhudumai wagonjwa wetu.” – Dkt. Mbwanji

Aidha Dkt. Mbwanji ameongeza kwa kusema sekta ya Umma na sekta binafsi zina kila sababu ya kufanya kazi kwa pamoja kwa lengo kumuhudimia mwananchi na hivyo hata  kupelekea kukua kwa sekta ya tiba utalii kwa wageni kutoka nje kuja kupata huduma za matibabu nchini kutokana na upatikanaji wa huduma bora za afya kupitia ushirikiano huo.

Kwa upande wake Dkt. Sisawo Konteh, Mkurugenzi Mtendaji wa Hospali ya Aga Khan Tanzania amepongeza makubaliano hayo kwani ni faida ya pande zote mbili kutokana na ukaribu wa kiutendaji wa kimkakati utakao kuwepo katika maeneo mbambali ikiwemo utoaji wa huduma za afya pamoja na kujengeana uwezo  kupitia ubunifu mbalimbali wa kitalaamu.

“…nipende kusema tunajivunia sana uwepo wa makubaliano haya yaliyofanyika kwani yatakuwa na faida kwa pande zote mbili katika maeneo mbalimbali kupitia kujengeana uwezo pamoja uwepo wa ubinifu mbambali kutoka kwa wataalamu wa pande zote mbili.” – Sisawo Konteh

Awali akiongea na waandishi wa Habari, Dkt. Mbwanji aliwataka wananchi kuendelea kujiunga na Bima ya Afya kwa wote ili kuepuka gharama zinazoweza kujitokeza pindi wanapopata changamoto ikiwemo magonjwa.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!