Latest Posts

MARTINA CHAMBIRI MJUMBE WA NEC MSTAAFU AFARIKI ALILIWA NA WENGI

 

Na Helena Magabe Tarime.

Marehemu Mama Martina Chambiri Mkongwe wa siasa ambaye enzi za uhai wake aliwahi kushika nyadhifa mbali mbali kwenye chama cha mapinduzi (CCM) alifariki machi 8,2025 na kuzikwa
kwa heshima na chama jana Machi 13,2025 nyumbani kwake mtaa wa Bomani wilayani Tarime .

Mama Martina Chambiri alizaliwa Novemba 28,1942 Shirati Wilayani Rorya katika historia yake alifanikiwa kusoma kozi mbali mbali na kuajiriliwa rasmi 1965-1970 Afisa maendeleo ya Jamii Musoma,1970-1978 Katibu wa UWT Wilaya,1978-1983 Afisa maendeleo ya Jamii (CDO) na Afisa maarifa ya nyumbani,1984-1987 katibu huduma za umma CCM Mkoa wa Mara,1987-1992 Katibu mwenezi CCM Mkoa wa Mara,1992-1996 Katibu wa CCM Mkoa wa Shinyanga baadaye Tabora 1992-1996 Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa(NEC)

Martina amefariki na umri wa miaka 83 lakini bado alikuwa na msaada kwenye chama kwani alikuwa mlezi na mjumbe wa mkutano mkuu Kata ya Bomani ambapo Mwenyekiti wa Mtaa wa Bomani ,Christina Joseph amewaomba WanaCcm husasani wa mtaa wa Bomani kuinga mfano wa Mama huyo ambaye hakuwahi kuyumba kwani alikitetea chama na kukilinda.

“Mimi huyu mama ndiye alinilea kwenye chama nikiwa Binti tangu 1997 akawa ananifundisha mpaka leo hii nina uwezo wa kuweza kusimama mbele za watu na kuongea ni kwa sababu yake alikuwa mtu mashuhuri kwenye mtaa mpaka mauti inamkuta alikuwa mlezi na mjumbe wa mkutano mkuu kata ya Bomani hakuwahi kuyumbishwa amekufa akiwa na damu ya CCM ” alisema Christina

Helena Bonyo amesema walianza siasa na Mama Martina Chambiri enzi za TANU alishika nyadhifa nyingi kwenye chama alikuwa na msimamo kwenye chama, alikuwa mshauri ambaye alikuwa akimsikiliza kila mtu na hata kama mtu alikosea kwenye chama alimrudisha kwenye mstari na aliruhusu mikutano mbali mbali ya wanachama mtaani kwake kufanyia nyumbani kwake.

“Huyu mama amekufa akiwa na damu ya CCM alikipenda sana chama tulianza naye toka enzi za TANU na Mimi nilikuwa huko hakuwa kigeugeu kwenye chama alikuwa anatuongoza vizuri hata ukiongea pumba anakurudisha kwenye mstari hata alivyokuwa maendeleo ya Jamii alikuwa anapambana tumepoteza mtu ambaye pengo lake haliwezi kuzibika” alisema Helena

Mwana Jumuiya ya Mt.Joseph Mfanyakazi Suzana Anicet amesema atamkumbuka Mama huyo kama moja wa waanzilishi wa Jumuiya ya Joseph Mfanyakazi ambayo baadae ilikuwa kubwa na kugawanywa ikapatikana jumuiya ya Mt Laurent ameongeza kuwa Mama huyo alikuwa mcheshi na mwenye upendo kwa kila mtu.

Kijana mkubwa Chacha Chambiri amesema wamepoteza Mama mwenye upendo mkubwa aliyewapenda watu na kufatia upendo huo kwa watu wote hakuwahi kufunga geti lake mchana ili mradi tu Mgeni yoyote anayefika nyumbani kwake aingie bila shida.

Mwenyekiti mstafu wa chama cha mapinduzi (CCM ) Mkoa wa Mara Samwel Kiboye amesema chama kimepoteza kiongozi muhimu na kiungo ndani ya chama ambaye hakupenda vurugu kwenye chama aliyependa kupatanisha watu ndani ya chama.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!