Latest Posts

MASHAMBULIZI YA ANGA YALIYOSHUKIWA KUTEKELEZWA NA ISRAEL YAANGAMIZA WATU 14 SYRIA

Takribani watu 14 wamepoteza maisha katika mashambulizi ya anga yaliyoshukiwa kufanywa na Israel dhidi ya Syria, kulingana na ripoti ya kituo cha habari cha BBC.
 
Mashambulizi hayo yamelenga maeneo matano, yakiwemo kituo cha utafiti wa kisayansi katika jimbo la Hama, magharibi mwa Syria.
 
Ndege za kivita za Israel zilishambulia maeneo ya kijeshi kwenye mji wa Masyaf, ambako wataalamu wanaounga mkono Iran walikuwa wakihusishwa na utengenezaji wa silaha.
 
Mfuatiliaji wa vita mwenye makao yake nchini Uingereza alieleza kuwa mashambulizi hayo yalitekelezwa kwa mawimbi kadhaa, yakilenga maeneo ya kijeshi yenye ushawishi mkubwa wa Iran.
 
Israel mara nyingi huwa haitoi maoni kuhusu mashambulizi yake ndani ya Syria, na haijatoa tamko rasmi kuhusiana na tukio hili. Hata hivyo, Israel imekuwa ikifanya mashambulizi mara kwa mara ndani ya Syria ili kuzuia ushawishi wa kijeshi wa Iran pamoja na makundi yenye silaha yanayofadhiliwa na Iran.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!