Latest Posts

MBEYA VIJIJINI KUGAWANYWA KUWA MAJIMBO MAWILI, MADIWANI WABARIKI

Na Josea Sinkala, Mbeya.

Baraza la madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Mbeya, limebariki mapendekezo ya kamati ya wataalam ya kuligawa jimbo la uchaguzi Mbeya vijijini na kupatikana majimbo mawili ya Mbeya na Mbalizi.

Akiwasilisha mapendekezo ya Halmashauri ya wilaya ya Mbeya kwa niaba ya Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri hiyo Bi. Erica Yegella, afisa utumishi wa Halmashauri ambaye pia ni mtendaji wa mji mdogo wa Mbalizi wilayani Mbeya Daudi Mbembela, amesema kikao kilichoketi kwa kushirisha wataalam mbalimbali, madiwani na chama kimependekeza jimbo la Mbeya vijijini ligawanywe kupata majimbo mawili.

Hii ni baada ya kupata barua kutoka ngazi ya Taifa kuruhusu mchakato wa kugawa au kubadilisha jina la jimbo juu ya kiu hiyo ya wana Mbeya vijijini.

Mbembela amesema mapendekezo yaliyotoka ni kugawa Tarafa ya Isangati na Usongwe kuwa jimbo la Mbalizi likijumuisha wananchi zaidi ya laki moja na kata kwamba zitakuwa zaidi ya thelathini huku jimbo tarajiwa la Mbeya likizaliwa kutoka Tarafa ya Tembela ambalo litakuwa na wananchi zaidi ya elfu tisini na kata zaidi ya kumi na tano.

Akichangia agenda hiyo mama ya kikao cha baraza maalum la madiwani, Diwani wa kata ya Iwindi Mhe. Admin Nfisile Nswila, amesema hiyo imekuwa haja na kiu yao kwa muda mrefu na wanaamini kugawa jimbo hilo ambalo ni kubwa kijiografia itasaidia kusogeza huduma kwa wananchi na kuchochea zaidi maendeleo.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Mbeya vijijini Akimu Mwalupindi, amewataka madiwani na wataalam kuendelea kuwa wamoja katika dhamira hiyo na kusisitiza kulinda maeneo ya Halmashauri ya wilaya yake hiyo kwa kutoruhusu kuchukuliwa maeneo yao kwenda eneo lingine la utawala katika Halmashauri/wilaya ambayo sio yao (Mbeya DC).

Akizungumza kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya Mbeya Mhe. Beno Morris Malisa, katibu tawala wilaya ya Mbeya m Mohamed Aziz Fakil, amewataka viongozi na wananchi kutokuwa na mashaka na kupokwa maeneo yao ya utawala kwani hoja zote zinajadiliwa vikaoni na kusisitiza Halmashauri hiyo kuendelea kusimamia ipasavyo ukusanyaji wa mapato kwa maendeleo ya wananchi.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Mbeya Mhe. Mwalingo Kisemba, ametumia fursa hiyo kumuomba mkuu wa wilaya ya Mbeya kuhakikisha hoja yao inapelekwa na kushughulikiwa kwa nguvu kwenye kikao cha ushauri mkoa (RCC) wa Mbeya, kutokana na ukubwa wa jimbo hilo.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!