Latest Posts

MBUNGE ATAJWA KUHUJUMU MKUTANO WA UVCCM BUKOBA VIJIJINI

 

Vijana wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) jimbo la Bukoba Vijijini wamelalamikia kukwama kwa baraza lao lililokuwa limepangwa kufanyika Kata Kemondo tarehe 26 Machi 2025 chini ya mwenyekiti wa UVCCM Mkoa Faris Buruha aliyeandaa kampeni ya (SANEVO) kwa mkoa mzima.

Wakiongea na Vyombo vya habari mara baada ya kutokea sintofahamu ya vurugu zilizotokea kutoka kwa vijana hao hadi kukwama kwa mkutano wameweka wazi kuwa wapo baadhi ya vijana ndani ya chama wanaotumiwa na mbunge wa jimbo hilo Jasson Rweikiza kukwamisha majukumu yao ya chama kama vijana chini ya Mwenyekiti Faris Biruhan jambo linalowasikitisha.

Ziara hiyo iliyoanza tarehe 10 mwezi huu imefanikiwa kuyafikia majimbo yote ya mkoa isipokuwa tuu Bukoba vijijini ilikokwama kutokana na mkwamo huo wa vurugu.

Akiongea kwa njia ya Simu Mbunge Wa Jimbo la Bukoba Vijijini Mhe Dkt. Jasson Rweikiza amekanusha kuhusika na tuhuma hizo kwa vijana hao kwani ndiye aliyewawezesha kuwapa ukumbi bure pamoja na vipaza sauti.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!