Latest Posts

MBUNGE NDAKIDEMI AGAWA MICHE BORA YA MIGOMBA 10,000 KATIKA KATA 14

Jumla ya miche 10,000 ya migomba bora,imegawanywa kwa Kata 14 za Jimbo la Moshi Vijijini ili kuhamasisha kilimo cha zao la ndizi na kuongeza uchumi wa familia.

Akigawa miche hiyo machi 31,2025 kwa Viongozi wa Chama cha Mapinduzi kutoka Kata 14 za Moshi vijijini zinazo fanya Kilimo Cha migomba ,Mbunge wa Jimbo la Moshi Vijijini Prof.Patrick Ndakidemi amesema kuwa miche hiyo itasaidia kukuza uchumi wa familia kutokana na migomba hiyo kuwa na uwezo wa kubeba mkungu wa ndizi wenye kilo 150 hadi 200 ikiwa itatunzwa vizuri hali itakayo chochea uchumi imara kwa wakulima wa zao hilo.

“Hii ilikuwa ahadi yangu niliyotoa kwa Wananchi na tokea nimekuwa Mbunge wao nimekuwa nikitoka Miche Bora ya migomba,kwasasa wakulima wamefaidika na wameanza kupeana migomba kwenye Jamii zao ili kupanua uwepo wa migomba Bora ya migomba” Prof.Ndakidemi

Amesema kuwa kwa sasa serikali inaelekea kufanya zao la ndizi kuwa zao la kibiashara hivyo wakulima wote wa Jimbo la Moshi Vijijini wanapaswa kufikiwa na miche hiyo ili adhima yake ya kuwepo kwa migomba bora itimie ili kufungua fursa kwa wote.

Ameongeza kuwa kwa sasa wanaandaa masoko ya kilimo na yapo maeneo ya kukusanya ndizi vijijini kuelekea katika masoko makubwa ya ndizi

Kwa upande wake Katibu wa wazazi wilaya Moshi Vijijini Andrew Mwando na Sofia Mshiu katibu wa CCM kata ya Mbokomu wamemshukuru Mbunge Ndakidemi kwa kutoa miche hiyo itakayo saidia kukuza uchumi na uhakika wa chakula.

Takribani miche bora ya migomba zaidi ya elfu 16 imesha tolewa na Mbunge huyo hadi sasa toka alipoanza kutumikia wananchi wa Jimbo la Moshi Vijijini ambapo wakulima wamefaidika na zao hilo na kufanikiwa kukuza uchumi wa familia zao.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!