Latest Posts

MBUNGE WA MOMBA AIBANA SERIKALI UJENZI BARABARA YA MLOWO

Mbunge wa jimbo la Momba Mkoani Songwe Mhe. Condester Sichalwe, ameihoji Serikali ni nini kauli ya Serikali juu ya ujenzi wa barabara ya Mlowo Utambalila hadi Kamsamba wilayani Momba kwa kiwango cha lami.

Akijibu swali hilo la nyongeza kutoka kwa Mbunge wa Momba, naibu Waziri wa ujenzi Mhandisi Godfrey Kasekenya, amesema Serikali imefikia hatua za mwishoni mwa kuanza ujenzi wa barabara ya Mlowo Utambalila hadi Kamsamba.

Naibu Waziri Kasekenya amesema Serikali kupitia wizara ya ujenzi ipo kwenye hatua za manunuzi (majadiliano na mkandarasi) na kwamba kabla ya kumalizika kwa mwaka huu wa fedha ni mategemeo yake kuona ujenzi huo ukianza kwa urefu wa kilomita 5 kutoka Mlowo na kilomita 5 nyingine zikianzia jimboni Momba.

Barabara ya Mlowo wilayani Mbozi hadi Kamsamba wilayani Momba ni barabara muhimu kwa wakati na wasafiri wa maeneo hayo kutokana na kutegemea shughuli za usafirishaji mazao na abiria pia lakini barabara hiyo imekuwa kikwazo kwa muda mrefu hivyo kujengwa kwa barabara hiyo kutaleta nafuu ya kiuchumi kwa wananchi na kuinua uchumi wa Taifa kwa ujumla.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!