Latest Posts

MBUNGE WA MSALALA ATOA ZAWADI YA NG’OMBE NA JEZI KWA VIJIJI 92 KWENYE MASHINDANO YA IDDI CUP

 

Mbunge wa Jimbo la Msalala, Mheshimiwa Iddi Kassim Iddi, ameshiriki kufunga fainali za mashindano ya Iddi Cup, yaliyofanyika katika Kata ya Mwakata. Katika fainali hiyo, mshindi wa kwanza alizawadiwa ng’ombe, huku timu ya Buyozi FC, iliyoshika nafasi ya pili, ikipokea zawadi ya shilingi laki mbili.

Mheshimiwa Iddi alieleza kuwa mashindano hayo yataendelea kufanyika katika kila kata ya jimbo hilo, ambapo kila mshindi wa kata atazawadiwa ng’ombe na shilingi laki mbili. Kwa ujumla, ng’ombe 18 na jumla ya shilingi milioni 3.6 zitatolewa kwa washindi wa mashindano hayo.

Mbali na hayo, mbunge huyo amegawa jezi na mipira kwa vijiji vyote 92 vilivyoshiriki ligi hiyo, huku gharama ya vifaa hivyo ikiwa takriban shilingi milioni 16.

Katika hotuba yake, Mheshimiwa Iddi Kassim Iddi alisisitiza kuwa juhudi hizi ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM), na zinaunga mkono jitihada za Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan katika kuendeleza michezo nchini.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!