Latest Posts

MC PILIPILI AMSIFIA RAIS SAMIA KWA KUMALIZIA DARAJA LA MAGUFULI, AANDAA SHOW YA “CHEKA KIDHAHABU” GEITA

 

Msanii maarufu wa sanaa ya uchekeshaji nchini, Emmanuel Mathias maarufu kama MC Pilipili, amewataka Watanzania kutambua na kuthamini juhudi kubwa zinazofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, katika kutatua changamoto mbalimbali za wananchi, ikiwemo kukamilisha miradi mikubwa ya maendeleo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo mkoani Geita wakati wa maandalizi ya onyesho lake la vichekesho la “Cheka Kidhahabu” linalotarajiwa kufanyika Aprili 21, MC Pilipili amesema moja ya mafanikio makubwa ni kukamilika kwa ujenzi wa Daraja la Magufuli ambalo amesema litakuwa msaada mkubwa kwa wakazi wa mikoa ya Geita na Mwanza.

“Ni muhimu Watanzania watambue namna Rais Samia ameendelea kuwekeza kwenye miradi mikubwa ya maendeleo. Kukamilika kwa daraja la Magufuli ni jambo kubwa sana kwa wananchi wa Kanda ya Ziwa,” amesema MC Pilipili.

Mbali na hilo, MC Pilipili amepongeza jitihada za serikali katika Mkoa wa Geita, akisema kuwa kumekuwa na maendeleo makubwa, hususan katika sekta ya elimu kupitia ujenzi wa shule na majengo ya ofisi za serikali yaliyojengwa kwa viwango vya juu.

Aidha, amebainisha kuwa mgeni rasmi katika onyesho hilo la “Cheka Kidhahabu” atakuwa Waziri wa Madini, Mhe. Antony Mafunde, sambamba na viongozi wengine mbalimbali wa serikali.

“Ni heshima kubwa kuwa na Waziri wa Madini kama mgeni rasmi kwenye tukio hili, ni ishara kuwa sanaa pia inatambuliwa kama sehemu ya maendeleo ya jamii,” amesema.

 

Onyesho hilo linatarajiwa kuvuta mashabiki kutoka mikoa mbalimbali, likiwa na lengo la kuleta burudani, kuhamasisha mshikamano wa kijamii na kuonesha namna sanaa inavyoweza kuchangia katika maendeleo ya Taifa.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!