Latest Posts

MCHAKATO WA KUWABAINI WATOTO WENYE SELIMUNDU WAANZA TABORA

 

Mkoa wa Tabora ni miongoni mwa mikoa nchi yenye idadi kubwa ya watoto wanaozaliwa na ugonjwa wa selimundu, ambapo Taasisi isiyo ya kiserikali ya Melian Foundation kupitia Wizara ya afya na Ofisi ya Raisi TAMISEMI imeanza kutoa huduma ya upimaji wa ugonjwa huo kwa watoto wanaozaliwa na kwenye vituo vya afya , kwa kuwabaaini na kuwapatia matibabu ili kukata mnyororo wa urithi wa ugonjwa huo huku pia wananchi wakitakiwa kuwapeleka watoto wao kwa ajili ya uchunguzi ili kuthibiti ugonjwa huo.

Hayo yameelezwa Mganga Mkuu wa mkoa wa Tabora Dkt. Honoratha Rutatinisibwa wakati wa uzinduzi mradi wa upimaji wa serimundu kwa watotomkoani Tabora , ambapo ulitanguliwa na utolewajii wa mafunzo kwa watumishi wa afya wa halimashauri pamoja na ugawiwaji wa vifaa tiba vitakavyo tumika katika kutoa huduma hiyo.

Kwa Upande wake, Mkurugenzi wa taasisi ya Melian, Samwel Mabewa ameeleza zoezi likavyofanyika ikiwemo utolewaji wa elimu ya namna kuwabaaini wagonjwa huku Mkurugenzi wa huduma za tiba kutoka Wizara ya afya, Daktari .Hamad Nyembea akiweka bayana hali ya ugonjwa huo kitaifa .

Nae, Katibu tawala mkoa wa Tabora Dkt. John Mboya, amewataka watumishi wa afya kuhakikisha watoto wachanga wanaozaliwa katika vituo hivyo wanawafanyia vipimo vya selimundu ili kuweza kuwabaini mapema na kuwapatia matibabu pamoja na kuhakikisha wanawafikia watu wote haswa waliopo pembezoni mwa miji .

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!