Latest Posts

MGAWANYO WA JIMBO MBEYA VIJIJINI WAZIDI KUBARIKIWA

 

Na Josea Sinkala, Mbeya.

Hoja ya kugawa jimbo la Mbeya vijijini imeendelea kupata baraka baada ya wajumbe wa baraza la ushauri wilaya ya Mbeya (DCC) kukubali jimbo hilo kugawanywa kutokana na ukubwa wa jiografia.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti kwenye kikao cha ushauri wilaya ya Mbeya, wajumbe hao wamesema jimbo hilo ni kubwa na limetimiza sifa nyingi za kupata jimbo lingine ili kuwa majimbo mawili hivyo kutaka mchakato huo kuchukuliwa kwa uzito hadi kwenye kikao kijacho cha baraza la ushauri mkoa (RCC) kwa hatua zaidi za ugawaji jimbo la Mbeya vijijini.

Akiwasilisha mapendekezo ya kamati ya wataalam na madiwani, afisa utumishi kutoka Halmashauri ya wilaya ya Mbeya ambaye pia ni mtendaji wa mamlaka ya mji mdogo wa Mbalizi Daudi Mbembela, amesema kusudi na pendekezo lililopo ni kugawa jimbo hilo kuwa na majimbo mawili ya Mbalizi litakalounganisha Tarafa ya Isangati na Usongwe na jimbo la Mbeya litakalotokana na tarafa ya Tembela.

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Mbeya vijijini Akimu Mwalupindi, amesema jimbo hilo ni kubwa hivyo wamekuwa wakikabiliwa na changamoto mbalimbali katika utendaji kazi hivyo kuendelea kuwaasa watumishi, viongozi wa kisiasa kuhakikisha maeneo yao yanalindwa kwa kutopokwa kwenda kwenye maeneo mengine ya kiutawala.

Mwenyekiti wa kikao hicho alikuwa ni Mkuu wa wilaya ya Rungwe Mhe. Jaffary Haniu kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya Mbeya Mhe. Beno Malisa, ambaye amesisitiza umoja na mshkamano kwa watumishi na wananchi wilayani Mbeya kwa ajili ya kuendelea kuwatumikia wananchi na kuhimiza ukusanyaji wa mapato katika Halmashauri ya hiyo.

Pia amesema maoni yaliyotolewa kwenye kikao hicho yamechukuliwa ili kwenda kuwasilishwa kwenye kikao cha ushauri mkoa RCC ili nao kuwasilisha ngazi za juu na kuwataka wana Mbeya vijijini kuendelea kuwa watulivu.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!