Mgodi wa Barrick North Mara umekabidhi Vitu mbalimbali ikiwemo mchele,mafuta ya kupikia Juice pamoja na Mbuzi katika kituo cha kulelea watoto waliokimbia kukeketwa cha ATFGM Masanga kilichopo wilayani Tarime Mkoani kuelekea sikukuu za Christmas na mwaka Mpya.
Kaimu Meneja idara ya uhusiano na mawasilisho Hermence Lula amesema kukikumbuka kituo hicho nakupeleka Faraja kwa Watoto waliokimbia kufanyiwa ukeketaji katika majumba yao hivyo wanaamini hiyo itakuwa furaja namba moja wanapoungana na wenzao kushiriki katika sikukuu hizo za mwisho wa Mwaka.
Akipokea mahitaji hayo Meneja Mradi wa kituo hicho cha ATFGM Masanga Valerian Mgani ameushukuru Mgodi huo kwa namna ambavyo umekuwa karibu najamii ambapo wanafanyia shughuli zao hivyo Daima hawatosau namna ambavyo wamekuwa sehemu ya Faraja.