Latest Posts

MHALIFU WA KIVITA LUBANGA AUNDA KUNDI JIPYA LA WAASI MASHARIKI MWA KONGO

Thomas Lubanga, mhalifu wa kivita aliyepatikana na hatia nchini Uganda, ametangaza kuanzisha kundi jipya la waasi Azimio la Mapinduzi (CPR) lenye lengo la kuiangusha serikali katika jimbo la Ituri, mashariki mwa Kongo.

Tangazo hilo linakuja wakati ambao jeshi la Kongo tayari linakabiliana na mashambulizi makali kutoka kwa waasi wa M23, kundi linalodaiwa kuungwa mkono na Rwanda.

Lubanga, ambaye ni mzaliwa wa Ituri, alihukumiwa na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) mwaka 2012 kwa kosa la kuwaajiri watoto askari. Alitumikia kifungo cha miaka 14 kabla ya kuachiwa mwaka 2020.

Baada ya kuachiliwa, aliteuliwa na Rais wa Kongo, Felix Tshisekedi, kuwa sehemu ya kikosi kazi cha kuleta amani Ituri. Hata hivyo, mwaka 2022, Lubanga alitekwa nyara kwa miezi miwili na waasi – hali anayodai ilipangwa na serikali. Tangu wakati huo, amekimbilia Uganda.

Katika mawasiliano yake na Shirika la Habari la Reuters, Lubanga amesema kuwa CPR ina matawi ya kisiasa na kijeshi, huku baadhi ya wanachama wake wakiwa na silaha katika maeneo matatu ya Ituri.

“Kuleta amani katika eneo hili kunahitaji mabadiliko ya haraka ya utawala na serikali,” amwsema Lubanga, lakini amesisitiza kuwa kundi lake bado halijaanza operesheni za kijeshi.

Haijulikani idadi ya wapiganaji walioko chini ya ushawishi wa Lubanga, lakini tayari wataalamu wa Umoja wa Mataifa walimshutumu mwaka jana kwa kuhamasisha wapiganaji kusaidia wanamgambo wa ndani na waasi wa M23.

Kuundwa kwa CPR kunazidi kuongeza mvutano wa kijeshi katika eneo ambalo limekumbwa na vita kwa miongo kadhaa, huku Kongo ikiendelea kupambana na makundi kadhaa ya waasi yanayodhoofisha juhudi za kuleta amani.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!