Latest Posts

MICHUANO YA GEUWASA MAJI CUP YAANZA KUTIMUA VUMBI MJINI GEITA

Michuano ya GEUWASA Maji Cup, inayodhaminiwa na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mjini Geita (GEUWASA), imeanza rasmi kwenye viwanja vya GGML, ikihusisha timu mbalimbali kutoka wilaya ya Geita.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa michuano hiyo, mgeni rasmi ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Geita, Hashim Komba, amesema mashindano haya yatatumika kama jukwaa la kutoa elimu kuhusu utunzaji na uhifadhi wa vyanzo vya maji.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chama cha Soka Wilaya ya Geita, Ally Twist, amepongeza juhudi za wadau wanaojitokeza kusaidia maendeleo ya soka katika eneo hilo. Naye, Mkurugenzi Mtendaji wa GEUWASA, Frank Changawa, amesema mashindano haya ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Maji, wakilenga kuhamasisha jamii kuhusu umuhimu wa rasilimali hiyo.

Katika mechi ya ufunguzi, timu ya Tiger FC iliibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya West Boy FC.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!