Latest Posts

MIREMBE KUTUMIA AKILI MNEMBA KUTIBU WAGONJWA WA AFYA YA AKILI

Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Afya ya akili,kutoka Hospitali ya Taifa ya afya ya akili Mirembe ,Dkt.Veronica Lymo amesema, wagonjwa wengi waliopo katika hospitali yao ni wale wenye umri wa kuanzia miaka 18 mpaka 40.

Dkt. Lymo ameyabainisha hayo Jijini Dodoma wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya afya 2025 yanayoendelea katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete na huduma  zinazotolewa na wataalamu bingwa na bobezi kutoka Hospitali za Mirembe, Benjamini Mkapa, Bugando, Moi, KCMC, Ocean Road, Kibong’oto.

Amesema miongoni mwa visababishi vinavyopelekea uwepo wa wagonjwa wengi wenye umri huo ni za kibailojia ama kisaikolojoa huku akidai vijana wenye umri wa kuanzia miaka 18  wanapitia changamoto nyingi ndio maana wapo kwa wingi katika hospitali hiyo.

Mbali na hayo amesema wamekuwa wakihamasisha wananchi jupima magonjwa hayo kwa kutoa elimu ambapo mpaka sasa wamezunguka katika mikoa mitano ili watu watambue nini maana ya afya ya akili, changamoto ya Afya za akili na magonjwa ya akili.

Aidha amefafanua kuwa utokana na uwepo wa teknolojia wako mbioni kuangalia namna ya kutumia akili mnemba katika utoaji wa huduma hasa katika  magonjwa ya afya ya akili.

Pia Dkt Lymo amewaasa wakazi wa Mkoa wa Dodoma kujitokeza kwa wingi katika kituo cha mikutano  Cha  Jakaya Kikwete  kwa ajili ya kufanya uchunguzi wa magonjwa mbalimbali ikiwemo ugonjwa wa afya ya akili.

“Tunawakaribisha wote kwa wingi hapa nia ni kuwasaidia ukipata msaada mapema unazuia shida ambayo ingetokea baadae,”amesema Dk Veronica.

Kwa upande wake Mkazi wa Dodoma Makulu Emmanuel Masawe amepongeza utoaji wa huduma na kuiomba serikali iwe endelevu kwa sababu kwenda hospitalini ni gharama na foleni ni kubwa, gharama kubwa wakati katika kituo cha mikutano cha Jakaya Kikwete wanatibiwa bure.

“Tunatamani Sana Kila Mtanzania aweze kufikia Jakaya Kikwete kupata huduma rafiki na nzuri hapa tunapima magonjwa yote ikiwemo Kupima mkojo pamoja na pressure,”

Ukifika Jakaya Kikwete utafanya upimaji wa Figo, Magonjwa ya Moyo na Mishipa, ⁠Upimaji wa Shinikizo la Damu  (BP) Ugonjwa wa Kisukari, Kifua Kikuu,Uzito na hali ya lishe,Huduma za Kinywa na Meno,Upimaji na matibabu ya Macho,Huduma za uzazi wa Mpango,Upimaji wa Saratani ya Matiti na Mlango wa Kizazi.

Chanjo ya Saratani ya Mlango wa kizazi (HPV),Msaada wa saikolojia na Afya ya Akili,Elimu ya Lishe, ⁠Upimaji wa Saratani

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!