Latest Posts

MNEC MEGITII: VIONGOZI CCM WAJITATHMINI

Viongozi wa Chama cha Mapinduzi CCM na wale wa Serikali wametakiwa kujitathmini kuhusu utekelezaji wa malengo waliojiwekea kwakua wananchi wanataka kuona mabadiliko kwa uhalisi na sio maneno bila vitendo.

Hayo yamebainishwa na mwenyekiti wa Halmashauri ya Bahi Mkoani Dodoma na MNEC, Donald Megitii, kuelekea miaka 48 ya CCM tangu kuanzishwa kwake nakuongeza kuwa katika shughuli mbalimbali Chama kimekua kikitoa maagizo ambayo viongozi wanapaswa kuyatekeleza kulingana na Ilani ya Chama hicho.

Ufunguzi wa shughuli mbalimbali zinazofanywa na Chama cha Mapinduzi (CCM) kuelekea miaka yake 48 zimefunguliwa rasmi leo katika Wilaya ya Bahi ambapo moja ya shughuli watakazofanya ni pamoja na kukagua miradi mbalimbali iliyotekelezwa Wilayani Chamwino Kata ya Ikoa kijiji cha Makoja.

MNEC huyo amesema Sherehe hizi za kihistoria zinatoa fursa muhimu kwa viongozi kukumbuka ahadi zao za kusimamia haki na ustawi wa jamii humuhimu wa kuimarisha haki na amani, akitahadharisha kwamba ni jukumu la viongozi kufanya kazi kwa karibu na wananchi ili kuhakikisha haki za kila mtu zinaheshimiwa

Megitii ameeleza kuwa CCM ni nguzo muhimu katika kuondoa dhuruma na unyanyasaji, huku akihimiza kuwa huduma za kijamii zinapaswa kuwafikia wananchi wote.

“Hii ni fursa ya kutathimini mafanikio na changamoto, huku mwaka huu ukiwa wa uchaguzi wa madiwani, wabunge, na Rais,”

Na kuongeza”Hivyo CCM inatarajia kushinda kwa kishindo, ikikumbuka lengo lake la msingi la kuwatumikia wananchi,” amesema Megitii.

Katika ujumbe wa matumaini, Katibu Mkuu wa CCM Mkoa wa Dodoma, Pili Mbaga, aliwaomba wananchi wa wilaya ya Chamwino kuhakikisha chama kinashinda tena kwa nguvu katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 2025.

“Kama tulivyofanya vizuri kwenye uchaguzi mdogo wa serikali za mitaa, ambapo tulishinda kwa asilimia 100 katika kata, vijiji, na vitongoji, basi tukafanye hivyo pia katika uchaguzi wa Rais, wabunge, na madiwani,” alisema Mbaga.

Kilele cha maadhimisho haya kinatarajiwa kufanyika tarehe 5 Februari katika Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma, ambapo viongozi na wanachama wa CCM watakusanyika kuadhimisha mafanikio na kuelekeza mikakati ya baadaye.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!