Latest Posts

MOTO WATEKETEZA SHULE KENYA, WANAFUNZI 17 WAFARIKI, SERIKALI YAANZISHA UCHUNGUZI

Wanafunzi 17 wamepoteza maisha baada ya ajali ya moto kutokea katika shule ya Hillside Endarasha, Kaunti ya Nyeri, Kenya, tukio hilo lilitokea usiku wa manane, wakati zaidi ya wanafunzi 150 walipokuwa wamelala kwenye bweni.

Moto huo, uliozuka mwendo wa saa sita usiku ulisambaa haraka kwa sababu majengo mengi ya shule hiyo yamejengwa kwa mbao.

Kwa mujibu wa Msemaji wa Polisi nchini Kenya, Resila Onyango, maafisa wa polisi wa uchunguzi wa jinai tayari wamefika eneo la tukio ili kuanza uchunguzi wa sababu za ajali hiyo. Katika tukio hilo, wanafunzi 14 walijeruhiwa na wanapatiwa matibabu kwenye hospitali za kaunti ya Nyeri.

Mkuu wa Polisi wa eneo hilo, Pius Murungu alithibitisha kuwa shule hiyo yenye jumla ya wanafunzi 824, wengi wao wakiwa na umri wa kati ya miaka mitano na 12, ilipoteza wanafunzi 17. Shule hiyo kwa sasa imefungwa wakati uchunguzi unaendelea.

Rais wa Kenya, William Ruto, ametuma salamu za pole kwa familia za walioathiriwa na kuahidi kuwa serikali itatoa msaada wa haraka kwa familia hizo. Pia ameagiza mamlaka kufanya uchunguzi wa haraka ili kubaini chanzo cha moto huo.

Kwa sasa, chanzo halisi cha moto bado hakijajulikana, lakini mamlaka zinaendelea na uchunguzi ili kubaini undani wa tukio hilo la kusikitisha.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!