Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2025 Ismail Ali Ussi amewataka wadau mbalimbali ikiwemo Taasisi na Mashirika binafsi kuwa wazalendo kwa kuanzisha miradi itakayoletea Taifa manufaa na ajira kwa wananchi na vijana
Ussi amebainisha hayo Wilayani Mvomero Mkoa wa Morogoro wakati azindua mradi wa kilimo misitu uliogharimu kiasi cha shilingi milioni 179 ambao umetembelewa na mbio za mwenge ambapo amesema kuwa kuanzisha miradi hiyo kutasaidia jamii kujikwamua kiuchumi
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Agriwezesha Deograsia Ignas amesema kuwa mradi wa kilimo misitu ulianza rasmi mwaka 2022 -2023 ambapo mpaka sasa miti zaidi ya miti laki sita imepandwa katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Morogoro.