Baraza la Wanawake mkoa wa Mtwara wamemuomba Mbunge wa Jimbo la Mtwara Mjini Hassan Mtenga kuwasaidia ujenzi wa kituo cha watoto yatima, Shule na ofisi.
Akitoa ombi hilo, Katibu wa Baraza la Wanawake mkoa wa Mtwara Aisha Suleiman wakati wa Iftar iliyoandaliwa na Mbunge huyo wa Jimbo la Mtwara Mjini amesema ni muhimu wakawa wa kituo maalumu kwa ajili ya watoto yatima ili wanapohitajika waweze kupatikana katika kituo chao.
“Tumejitahidi tumepata kiwanja katika viwanja vya Mji mwema eneo la Samia City, tunakuomba Mbunge ujitahidi ili watoto hawa wapate makazi maalumu pindi wanapohitajika wapatikane kwenye kituo chao”amesema Aisha
Ameongeza kuwa, “Lakini pia ututafutie wadau mbalimbali mana hutaiweza kazi hii peke yako lazima uwe na wenzako na tunakuombea uendelee kwenye miaka mitano mengine”
Hata hivyo Mbunge huyo ameuomba uongozi huo uweze kumuombea dua ili itakapofika mwakani (2026) aweze kuchangia asilimia 70 ya ujenzi huo.
Akizungumza kwa niaba ya watoto wenzake, Mwanasa Athumani amemshukuru mbunge kwa kuwakumbuka watoto hao na kuwaalika nyumbani kwake kwa ajili ya kufturu nao kwani wapo wadau wengi wenye uwezo ila wanafuturisha makundi mengine.
Mwwakilishi wa Mratibu wa watoto hao, Faizun Ahmad amesema jambo ambalo amelifanya Mbunge huyo ni la kuigwa na wadau wengine kwani wadau wengi wamekuwa wakiwasahau watoto yatima na wanaoishi kwenye mazingira magumu na kuongeza kuwa kufuturu na watoto hao ametia nuru kwenye nyumba yake.