Latest Posts

 MWENEZI BAWACHA AILIPUA SERIKALI HADHARANI,SAKATA LA WALIMU WA KUJITOLEA LAIBUKA “UKIONA WANALALAMIKA UJUE TUNAELEKEA KWENYE UKOMBOZI”

K

atibu Mwenezi wa Baraza la Wanawake wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (BAWACHA) taifa Sigrada Mligo ameitaka halmashauri ya wilaya ya Makete kutoa mikopo ya 10% haraka kwa vikundi vilivyokidhi vigezo bila kuleta urasimu wala sababu kwa kuwa ni haki ya watanzania kupata fedha hizo kwa kuwa ni kodi zao.

Sigrada ameeleza hayo mkoani Njombe wakati akizungumza kwenye mkutano wa hadhara na wananchi wa Makete uliofanyika katika eneo la sokoni Makete mjini ambapo amesema wananchi wamekuwa wakisumbuliwa na mikopo hiyo na kuwasababishia adha kubwa huku wakiwa wametumia fedha zao nyingi kukamilisha mchakato wa mikopo.

Aidha amewatanzania kutoka usingizini na kuacha kuwachukia wafanyabiashara wanaouza bidhaa kwa gharama kubwa kwa kuwa bidhaa kupanda bei kunatokana na usimamizi mbovu wa kikodi unaosababishwa na serikali iliyopo Madarakani.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!