Latest Posts

NAIBU WAZIRI KIHENZILE : SEKTA BINAFSI IONGEZE KASI YA UWEKEZAJI KWENYE USAFIRI WA ARDHINI

Naibu Waziri wa Uchukuzi, Mhe. David Kihenzile, ametoa wito kwa Sekta Binafsi kuongeza kasi ya uwekezaji katika uendeshaji wa usafiri wa ardhini ili kuchochea ajira na kuongeza kipato kwa Watanzania.

Ametoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam wakati akifungua maonyesho ya Wiki ya Usafiri Endelevu Ardhini yaliyofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, kwa niaba ya Waziri wa Uchukuzi, Profesa Makame Mbarawa, na kusema kuwa Serikali imeendelea kufanya maboresho ya sheria na kanuni yanayolenga kuboresha mazingira ya utoaji huduma za usafiri nchini.

“Katika kipindi cha miaka minne Serikali imefanya maboresho makubwa, kuanzia sheria za usafirishaji hadi uwekezaji wa miundombinu, na matokeo ya kazi hizi yanaonekana kwa kila mtu leo” alisema.

Kihenzile alizitaka taasisi zinazotoa elimu ya katika maonyesho hayo kuendelea kuelimisha jamii kuhusu umuhimu wa kutunza na kulinda miundombinu ili uwekezaji mkubwa uliofanywa na Serikali uwe na manufaa kwa Watumiaji.

Kwa upande wake, Raymond Shoniwa
Mkurugenzi Mtendaji Southern African Railway Association (SARA) ameipogeza Serikali kwa hatua kubwa iliyofanya katika kuboresha miundombinu, hususan reli ya kisasa (SGR), akizitaka nchi nyingine kuja kujifunza namna Tanzania ilivyopiga hatua katika sekta hiyo.

Naye Mkurugenzi wa Maji wa Mamlaka ya Usafiri Ardhini (LATRA), CPAT Habib Suluo, alisema mamlaka imejipanga kuhakikisha mazingira ya utoaji huduma kwa watumiaji na wamiliki wa vyombo vya usafiri yanakuwa salama, bora na ya uhakika wakati wote.

Maadhimisho ya Wiki ya Usafiri Endelevu ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Usafiri Endelevu Duniani, ambayo hufanyika kila tarehe 26 Novemba. Kwa mwaka 2025, maadhimisho haya yamebeba kaulimbiu “Nishati Safi na Ubunifu katika Usafirishaji.”

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!