Latest Posts

NAIBU WAZIRI WA BIASHARA NA VIWANDA AWATAKA WATANZANIA KUANZA KUPENDA BIDHAA ZAO


-Asema Wakenya wametutangulia Kwa kila kitu.

-Asema mkoa wa Mara haukutendewa haki kwenye sekta ya mifugo na uvuvi.

-Ataka thamani ya mazao na mifugo kuongezeka ataka ziwekwe tozo rafiki kwa wafanyabiashara .

Naibu waziri wa Biashara na Viwanda Mhe Exaud Kigahe amewataka wananchi kuanza kupenda kwanza bidhaa zao kwa kuzipa thamani ili kudhibiti vipenyo vya kuvusha bidhaa kwenda nchi jirani ya Kenya kutafuta soko zuri.

Hayo ameyasemwa Tarime alipotembelea mpaka wa Kenya na Tanzania ambapo amesema Mkoa wa Mara ni mkoa wa kimkakati kama ilivyo mikoa mingine iliyopo mipakani lakini viwanda vyake vyote vimekufa lakini vinatakiwa kufufuliwa na kulindwa ambapo amesema si afya kwa uchumi wetu kununua mafuta ya kula nchini Kenya wakati tuna kiwanda chetu cha mafuta ya alizeti kilichopo wilayani Rorya.

“Wenzetu wametutangulia kwa kila kitu inatakiwa viongozi mfanye kila muwezalo kuhakikisha mnawasaidia wafanyabiashara kushindanisha bidhaa zao ili wathamini ubora wa bidhaa mhakikishe mnajenga sekta binafsi muwaondolee tozo zisizo rafiki kwani mpaka wa Sirari una fursa sana kuna ng’ombe bora nyama hata kama haijasindikwa tuangalie ubora na kuishindanisha ” alisema Kigahe

Mkuu wa wilaya Tarime Meja Edward Gowele amesema mpaka ni mkubwa hivyo changamoto ni kuna vichochoro vingi vinavyotumika kuvusha mazao kwa njia ya magendo kuingia Kenya lakini kwa kuwa soko la mkakati la kimataifa la mazao lililokwama toka 2014 sasa limeanza kujengwa baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kutenga fedha kwaajili ya soko hilo na pindi litakapokamilika litasaidia wakulima kuuza mazao yao kwa bei nzuri.

katibu Tawala Mwalimu Saul Mwaisenye amesema hata uwekwe ulizi wa aina gani hata ujengwe ukuta bila kuweka bei rafiki za bidhaa ni kazi bure ambapo ametolea mfano wa simenti ya Tanzania inauzwa elfu 23000 hadi 26000 kwa mfuko wakati simenti ya Kenya inauzwa elfu 19000 hadi 20,000 kwa mfuko na kushauri viwanda visogezwe karibu.

Mwenyekiti wa Halmashauri Tarime Vijini Simon Kilesi ambaye ni mfanyabiashara na ni wakala wa sukari amesema soko la sukari la Tanzania liko juu kuliko Kenya kutokana na umbali wa sukari inayotoka Tanzania lakini sukari ya Kenya iko karibu.

Amefafanua kuwa sukari inayotoka Kenya ni ya magendo ambapo amesema kuwa viwanda vya Kenya vikifunguliwa sukari inakuwa chini sana vikifungwa vikafunguliwa vya Tanzania inakuwa juu inauzwa ndani lakini na Kenya inaifata ila hana hakika kama wanalipia ushuru.

Afisa mkaguzi wa mazao Philipo Emmanuel Lusotole amesema Kenya wana uwezo wa kuchukua sukari iliyoharibika na kuweka rebo ya kuiongezea muda mbele na kuiunza na hayo ni madhara ya magendo hivyo njia rahisi ya kupambana na magendo ni kujenga kiwanda cha sukari Tarime.

Kaimu meneja forodha Abdala Mambi amesema idara ina tasisi 19 ndani yake ambapo imeajili watumishi 91 lakini Kuna changamoto ya magendo lakini wamejitahidi kutoa elimu mara jwa mara kwa kutumia kitengo cha kudhibiti magendo lakini bado changamoto ni kubwa kwani mpaka ni mkubwa wenye kilometa 17.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!