Latest Posts

NANDONDE: CHADEMA PWANI YAANZA KWA KISHINDO UJENZI WA OFISI YA MKOA

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mkoa wa Pwani kimeanza kwa kasi utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa ofisi ya chama hicho mkoani humo, ambao kwa sasa uko katika hatua za msingi na unaendelea vizuri.

Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi, Baraka Nandonde, amethibitisha kuwa mafundi wameshaingia eneo la mradi lililopo Mathias, wilayani Kibaha mkoani Pwani, na kazi inaendelea.

Akizungumza na Jambo TV kwa njia ya simu, Nandonde amesema:

“Ujenzi upo hatua ya msingi, na kila kitu kinaendelea vizuri. Tunahakikisha kuwa kazi hii inakamilika kwa wakati na kwa viwango vinavyohitajika.”

Nandonde, ambaye ni mwenyekiti wa zamani wa CHADEMA Mkoa wa Pwani na aliyewahi kugombea nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Kanda ya Pwani, ameeleza kuwa kamati yao inatamani ofisi hiyo izinduliwe na Mwenyekiti mpya wa Taifa atakayechaguliwa katika uchaguzi mkuu wa chama unaotarajiwa kufanyika mapema mwakani.

Aidha, amewataka wadau wa chama hiko, wanachama, na wapenda maendeleo kushirikiana na kamati yao katika kuhakikisha ujenzi huo unakamilika kwa mafanikio.

“Tunatoa wito kwa kila mmoja kuchangia kwa namna anavyoweza. Hii ni hatua muhimu kwa chama na mkoa wetu,” alisisitiza.

Ujenzi wa ofisi hiyo ni miongoni mwa jitihada za CHADEMA kuhakikisha inaimarisha miundombinu yake katika ngazi za mikoa, huku ikiwa ni ishara ya kusimama imara kwa chama hicho kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.

Ofisi hiyo inatarajiwa kuwa kitovu cha kuimarisha utendaji kazi wa chama katika Mkoa wa Pwani.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!