Latest Posts

NI MAFURIKO YA TUNDU LISSU ELIMU YA NO REFORMS NO ELECTION

Na Josea Sinkala, Songwe.

Utitiri wa wanachama na wananchi umeendelea kushuhudiwa kwenye mikutano ya hadhara ya mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Tundu Antipas Lissu, ambapo ijumaa hii ameendelea na mikutano ya hadhara na vikao vya ndani mkoani humo.

Maelfu ya wananchi wamejitokeza kwenye miji ya Vwawa na Mlowo mkoani Songwe kwa ajili ya kusikiliza agenda ya CHADEMA ya No reforms no Election ambapo CHADEMA inashinikiza ubadilishaji wa sheria za uchaguzi na tume huru ya uchaguzi ambayo itawajibika kwa wananchi.

Akizungumza na wananchi mjini Vwawa na baadaye mji mdogo wa Mlowo wilayani Mbozi mkoani Songwe, Tundu Lissu mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, ameeleza madhaifu mbalimbali yanayojitokeza kwenye chaguzi zinazosimamia na mkono wa Serikali akisema zimeacha majeraha mengi na kugharimu maisha ya watu mbalimbali huku wapinzani wakidaiwa kushindwa kwenye chaguzi hizo.

Lissu amesema mfumo wa sasa wa uchaguzi una mlengo wa chama kimoja ambacho ni chama tawala hivyo kuwataka wananchi kuwaunga mkono CHADEMA kwa kuhakikisha uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 haufanyiki kutokana na sheria kandamizi zihusuzo masuala ya uchaguzi na kukosa tume ambayo ina uhalisia na uhuru wake.

Sanjari na hayo amelitupia lawama jeshi la Polisi kwa madai kuwa wengi wao wamekuwa wakitumika vibaya kwenye usimamiaji uchaguzi, walimu pamoja na maafisa watendaji hoja iliyoungwa mkono pia na mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Songwe Isakwisa Lupembe.

Kwa upande wake mwenyekiti wa CHADEMA kanda ya Nyasa Joseph Mbilinyi (Sugu) ameeleza kuendelea kuhimiza wananchi katika kanda yake kuhakikisha uchaguzi huo mkuu haufanikiwi akisema kwa asilimia kubwa mazingira yanaibeba CCM kuonekana washindi kwenye chaguzi mbalimbali licha ya vyama vya upinzani hasa CHADEMA kuibuka kidedea.

Makamu mwenyekiti wa CHADEMA kanda ya Nyasa Frank George Mwakajoka, amelitaka jeshi la Polisi kutojihusisha na masuala ya uchaguzi wakati ukiwadia akisisitiza kuwa CCM ya sasa ina uongozi uliofitinika.

Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Tundu Lissu akiwa ameambatana na viongozi mbalimbali akiwemo askofu Emmaus Mwamakula na mwanaharakati Mdude Nyagali, anaendelea na mikutano ya hadhara katika maeneo mbalimbali katika kanda ya Nyasa ambapo amefanya katika mikoa ya Mbeya, Rukwa na Songwe huku makamu mwenyekiti wa CHADEMA (Bara) John Heche akifanya mikutano hiyo katika majimbo na wilaya za Rungwe, Kyela, mkoa wa Njombe na Iringa ambapo baadaye Machi 30, 2025 CHADEMA itahimisha mkutano wa pamoja na viongozi wote hao wa kitaifa mkoani Iringa kwa kufunga ufunguzi wa kampeni ya No Reforms No Election katika kanda ya Nyasa kisha kuelekea kanda nyingine kueneza agenda yao hiyo.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!