Februari 27, 2025 – Mara
- Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Chadema (BAVICHA) Mkoa wa Mara Ndg. Alphonce Machira amezungumza na mwandishi wa Jambo TV kuhusu maoni yake ambayo amekuwa akisikika katika maeneo mbalimbali ya majukwaa ya kisiasa juu ya kauli zake za kupendekeza wilaya ya Rorya kugawanywa majimbo mawili ya kiuchaguzi,
Jambo Tv ilipomuuliza kwanini anafikiri Rorya inapaswa kuwa na majimbo mawili ya kiuchaguzi ikiwa kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2022 wilaya ya Rorya ilikuwa na wakazi wasiofika laki tatu na nusu huku kwa mujibu wa sheria, kanuni na Utaratibu wa ugawaji wa majimbo moja ya kigezo ni kuwa na idadi ya watu wasiopungua laki nne,..
Machira aliweka utetezi wake akisema,..
“Tukipitia vigezo vya Ugawaji wa majimbo, binafsi naona ni vyema Rorya Iweze Kugawanywa kua na majimbo mawili ya kiuchaguzi maana ukiangalia kigezo Cha ukubwa wa eneo, Rorya ni moja ya majimbo ambayo eneo lake la kiutawala ni kubwa sana, Rorya Ina Kata 26, Vijiji 87, Vitongoji 508 na hivyo Vijiji, Kata , na Vitongoji sio Vya Karibu Karibu”…
Machira aliongeza kwa kusema,
“Mfano kutoka Kata ya Nyamunga hadi Kata ya Iloma ni umbali mrefu sana, ni mahala ambapo unatumia nauli ya shilingi 30,000 kwa usafiri wa Pikipiki, yaani utafikiri unatembea ndani ya mkoa kumbe uko upo ndani ya Jimbo moja, na ukitoka Kata ya Bukuta Kijiji cha Kirongwe hadi Kata ya Rabuor ni kama vile unatembea ndani ya mkoa kumbe bado upo ndani ya Jimbo moja. na ukitoka Pale kata ya Nyathorogo kule KISUMWA hadi kule ziwani Sota kata ya Tai ni kama Vile unatembea ndani ya majimbo mawili Ya Tarime Mjini na Tarime Vijijini”
Mwandishi wetu alimuuliza tena, Je, maelezo hayo ya ukubwa wa kimaeneo pekee anahisi inatosha sasa Rorya katazamwa kwa jicho la mapendekezo yake?..
Machira Alijibu,…
“Ndio kwa ukubwa huu na aina ya Gharama Inayotumika ndani ya jimbo moja, inapelekea Wananchi wa Rorya Kuna wakati wanakosa huduma ya haraka kwa kigezo cha ukubwa, Utoaji wa huduma Unakua mgumu kwa wawakilishi kwasababu ya hiyo hali, lakini pia Kwa ukubwa huo unapelekea hata uchaguzi wa viongozi ufanywe kwa kuzingatia pesa zao Kuliko uwezo wao maana bila kua na pesa kuzunguka Rorya nzima ni changamoto sana..
Jambo Tv ilihitaji kufahamu hali ya uchumi kwa watu Rorya iko vipi,..
Machira anaendelea,..
“Ukiangalia kigezo cha uwezo wa kiuchumi, Rorya ina Ziwa Victoria na inazalisha sana, mwambao mwa Ziwa Victoria kuna uzalishaji wa samaki kwa asilimia kubwa, mfano Miaro ya Busurwa, Kanga, Sota , Rwang’enyi, Bubombi, Kirongwe na maeneo mengine kuna uzalishaji mkubwa sana, sio hivyo tu, Rorya kuna minada mikubwa Ikiwemo Randa, Shirati, Nyamaguku , Mariwa, na maeneo mengine, hivyo Kuna Uzalishaji Wa Kiuchumi, Rorya kuna shughuli za kiuchumi Kupitia Kilimo na Wananchi wako tayari kupigania Rorya kwa shughuli hizi na kukuza uchumi Wa Rorya”..
Jambo Tv, ilimuuliza juu ya kigezo cha Mipangilio ya mji kwa Rorya ukoje na ukubwa wake kimaeneo,..
Machira alifafanua zaidi,..
“Kigezo cha mpangilio wa maeneo, Rorya maeneo yake bado yako wazi na mipango miji jnaweza kuipanga Vyema, lakini pia mpaka sasa Vijiji ndani ya Jimbo la Rorya vinakua kwa kasi sana ni jambo la msingi sana kuwafikia wananchi, kigezo hiki Rorya Imekidhi Kwa asilimia kubwa sana”
Jambo Tv, Usalama wa njia za kimawasiliano wilaya ya Rorya upoje?..
“Kigezo cha upatikanaji wa njia ya mawasiliano, Rorya inaingilika kwa njia zote, kuanzia ardhini hadi majini, mpaka sasa kupitia Bandari ya Kinesi watu wa Musoma wanaingia Rorya, na kupitia pia Barabara Rorya Inafikika kwa pande zote kuu nne za Dunia, pia Rorya ikigawanywa Barabara zitaongezeka na Wananchi watapata huduma ya Barabara na mawasiliano mengine kwa haraka sana”
Jambo Tv, Umezungumza lakini haujagusia kabisa suala la idadi ya wakazi wa Rorya?
Majibu ya Machira,..
“Nikweli imeandikwa kua inatakiwa kuwe na Watu 400,000 na kwa mujibu wa Sensa ya mwaka 2022 Rorya kuna 350+, pamoja na wanaRorya kua na watu laki tatu hamsini zaidi hii kwangu sio hoja ya Kutoigawa Rorya, Ikumbukwe suala la idadi ya watu ni ‘Dynamic’ inabadilika badilika sana, huenda kwa sasa na baada ya miaka mitatu ijayo tayari tukawa tumeshaafika, lakini hata hivyo mbeleni kufikia 2032 tutakua tumeshaafika Hao watu laki Tano na ushee kwahiyo kwangu mimi hii siyo hoja yakufanya Rorya Isigawanyawe, na moja ya msukumo wa ‘No Reforms na Election’ ni pamoja na Rorya kupatiwa majimbo mawili ya uchaguzi..