Latest Posts

NYAMANDEGE ATETEA KITI CWT MUSOMA VIJIJINI 

 

Aliyekuwa mwenyekiti wa Chama cha Walimu Wilaya ya Musoma Vijijini Mussa Nyamandege amefanikia kutetea kiti chake cha Mwenyekiti baada ya kuibuka Mahindi wa Kura 71 kwa 48 dhidi ya mpinzani wake wa karibu Brighton Katondo ambaye amepata Kura 48

Akitangaza Matokeo hayo msimamizi wa Uchaguzi ambaye pia nimwenuekiti wa Chama cha walimu Mkoa wa mara Abdallah malima akamtangaza Mussa Nyamandege kuwa ndio Mwenyekiti wa CWT Wilaya ya Musoma.

Akizungumza mara baada ya Matokeo hayo mwenyekiti mpya wa CWT amewataka wanachama kuwa wamoja na kuwa Uchaguzi huo usitumike kuwagawa wanachama badala yake ukawajenge kuwa kitu kimoja katika kuhakikisha wanatetea masirahi yao na kutatua changamoto zinazowakabili walimu.

“Twendeni tukavunje kambi zetu najua kulikuwa na kambi sasa Uchaguzi umeisha twendeni tukafanye kazi kwa maslahi ya watoto wetu na Sisi wenyewe na Taifa kwa ujumla”Mussa Nyamandege mwenyekiti wa CWT Musoma Vijijini.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!