Tumejifunza kuwa hizi nguo zinazozalishwa na kiwanda kilichopo eneo la Mamlaka ya Eneo Huru la Uwekezaji kwa Mauzo Nje (EPZA) hususani hizi ‘jeans’, wateja wake wakubwa ni watu wa nje ya nchi hasa Marekani, kwa hiyo wale wanaodhani kuwa Tanzania hatuwezi kuzalisha bidhaa zikaenda zikauzwa nje, sisi leo tumejionea kwa macho yetu na tunaona kwamba ni kwa kiasi gani Tanzania inaweza kuzalisha bidhaa ndani ya Tanzania na soko kubwa nje ya nchi hasa katika taifa kubwa kama Marekani”- Mwanaasha. Mwenyekiti wa Kamati ya Bajeti na Fedha ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar Bi Mwanaasha Khamis Juma, yeye na kamati yake walipotembelea Mamlaka ya Eneo Huru la Uwekezaji kwa Mauzo Nje (EPZA) Alhamisi Aprili 18, 2024 na kufanya kikao kilichoongozwa na Mkurugenzi wa Idara ya Uhamasishaji na Uwezeshaji Uwekezaji EPZA James Maziku, kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa EPZA Charles Jackson Itembe.