Latest Posts

ONGEZEKO LA JOTO NI TISHIO NCHINI

 

Serikali imezindua mradi wa miaka mitatu wa utoaji taarifa za tahadhari kuhusu matukio ya hali mbaya ya Hewa huku takwimu zikieleza kuwa kwa mwaka 2024 joto limeongezeka kutoka nyuzi joto 23.6 hadi 24.3 hali ambayo haijawahi kutoka katika historia Nchi.

Uzinduzi huo wa Mradi unaotambulika kama ‘Early Warning for All’ ama kwa tafsiri isiyo rasmi kuwa Tahadhari za mapema kwa wote, umefanyika leo Jumatano Machi 19,2025 Jijini Dodoma na Naibu waziri wa Uchukuzi David Kihenzile.

Amesema mabadiliko ya Hali ya hewa yamezidi kuwa na athari kubwa mwaka hadi mwaka nakuongeza kuwa kwa mwaka 2024 ni mwaka ambao mvua kubwa ilinyesha hadi kufikia milimita 316 ndani ya masaa 24.

Lengo la Mradi huo ni kupanua wigo wa Taarifa nakuweza kuwafikia Watu wote hususani wanaoishi Vijijini Kwakuwasaidia kuchukua tahadhari za mapema kabla ya kutokea kwa majanga yatokanayo na mabadiliko ya hali mbaya ya hewa na tabia ya Nchi pamoja na kuokoa maisha ya watanzania na mali zao.

Mradi huo unatekelezwa na Mamlaka ya hali ya hewa Nchini TMA kwa ushirikiano na wadau mbalimbali wa ndani na nje ya nchi ikiwa ni mwitikio wa maelekezo ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuwa ifikapo 2027 kila mtu anafikiwa na taarifa za tahadhari ya hali mbaya ya Hewa.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!