Latest Posts

POLISI LUDEWA YAZUIA MKUTANO WA MWENEZI BAWACHA TAIFA

Jeshi la Polisi wilaya ya Ludewa mkoani Njombe limezuia mkutano wa hadhara wa Mwenezi wa Baraza la Wanawake wa CHADEMA (BAWACHA) Taifa uliotakiwa kufanyika Ludewa mjini kwa madai ya kuwa ni maelekezo kutoka juu.

Akizungumza na Jambo TV mara baada ya kuzuiwa kwa mkutano huo Hamid Mfalingundi ambaye ni Naibu katibu wa BAZECHA Taifa Tanzania bara anasema jambo hilo limewasikitisha kwa kuwa maandalizi yalikwishafanyika mpaka wamefika wilayani humo.

“Ni jambo la ajabu kabla ya mkutano tumefuatwa na OCCID na kutuzuia kwamba hatupaswi kufanya mkutano huo tukahoji ni kwanini hatupaswi kufanya mkutano halali wa kisiasa akasema ni maagizo kutoka juu”amesema Mfalingundi

Kwa upande wake Sigrada Mligo ambaye ni Mwenezi wa Baraza la Wanawake Taifa (BAWACHA) amelaani kitendo hicho kwa kuwa hakuna jambo la hatari ambalo Chama hicho kinafanya.

“Ninachotaka kusema ni kuwa wameanza kuogopa mapema mno,halafu huu mkutano wa CHADEMA una nini cha hatari ambacho kingefanyika na kufanya jeshi la Polisi lishindwe labda kusimamia ebu mtuachie hiyo hofu inatoka wapi?”amesema Sigrada.

Kwa upande wake John Mapunda mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Ludewa anasema walifikisha taarifa za mkutano huo siku tatu zilizopita lakini ghafla jeshi la Polisi limezuia mkutano wao huku tayari wameshaingia gharama.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!