Latest Posts

POLISI NA MGONJWA WAUAWA KWA RISASI HOSPITALINI MEXICO

Watu wenye silaha walivamia hospitali nchini Mexico Jumatatu na kumshambulia mtu aliyekuwa akipona jeraha la risasi, na kumuua yeye pamoja na maafisa wawili wa polisi, mamlaka zimesema.

Kwa mujibu wa Citizen Digital, washambuliaji walimpiga risasi mtu huyo zaidi ya mara 10 katika mji wa katikati wa Atlixco, kisha kuwaua maafisa wa polisi waliojibu shambulio hilo na kujaribu kuwazuia kutoroka, kulingana na sekretarieti ya usalama wa umma katika jimbo la Puebla.

“Aliyekuwa mwathirika aliingia hospitalini mapema Jumapili akiwa peke yake, kwani alikuwa amejeruhiwa kwa risasi katika mkusanyiko,” amesema Katibu wa Usalama wa Puebla, Daniel Ivan Cruz, katika mkutano na waandishi wa habari.

“Mapema Jumatatu asubuhi, mtu huyo aliuawa na wanaume kadhaa waliovamia hospitali hiyo. Baada ya kupokea simu ya dharura na kufika eneo la tukio, polisi walipigwa risasi na kufariki papo hapo,” amesema.

Wachunguzi walikuwa wakichunguza iwapo mgonjwa huyo, aliyekuwa na umri wa miaka takriban 30 alikuwa akijihusisha na shughuli haramu, sekretarieti ya usalama ilisema.

Atlixco, ambao ni kivutio maarufu cha watalii, hupokea maelfu ya wageni wakati huu wa mwaka kwa ajili ya sherehe za Siku ya Wafu.

Ukatili unaoongezeka, ambao mara nyingi unahusishwa na biashara ya dawa za kulevya na magenge, umesababisha zaidi ya watu 450,000 kuuawa nchini Meksiko tangu mwaka 2006.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!