Latest Posts

POLISI TANGA WAIMARISHA ULINZI SIKUKUU ZA EID NA PASAKA

Jeshi la Polisi Mkoa wa Tanga limesema limejipanga kikamilifu kuimarisha doria katika kipindi cha sikukuu za Eid na Pasaka, kwa lengo la kudhibiti vitendo vya uhalifu vinavyoweza kujitokeza na kuhakikisha usalama wa raia na mali zao.

Kauli hiyo imetolewa na Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Tanga, Alimachius Mchunguzi, akisema kuwa wamejipanga kuimarisha ulinzi katika maeneo mbalimbali ikiwemo kumbi za sherehe, fukwe za bahari pamoja na nyumba za ibada, ili kuhakikisha usalama wa wananchi katika kipindi chote cha sikukuu.

Pamoja na hayo, Kamanda Mchunguzi ametoa rai kwa wananchi wa Tanga, hususan wazazi, kuhakikisha wanakuwa waangalizi wa watoto wao, hasa wanapokwenda katika maeneo ya starehe, ili kuepusha madhara yanayoweza kujitokeza.

Aidha, Kamanda Mchunguzi amesema Jeshi la Polisi Mkoa wa Tanga halitasita kumchukulia hatua za kisheria mtu yeyote atakayehusika na vitendo vya kihalifu.

 

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!