Theophilida Felician, Kagera.
Wanachama wa taasisi ya ubalozi wa amani PPA mkoa Kagera wamechukua hatua ya kujifunza mafunzo mbalimbali yanayolenga kuitunza na kuilinda amani.
Wanachama hao ambao wanaendelea na somo la Moduli ya amani na uzalendo katika jamii wanasoma na kujifunza mambo muhimu yaliyomo ndani ya moduli hiyo iliyoandaliwa na watalaamu wa taasisi hiyo.
Mada zilizohusika katika mafunzo yaliyofanyika manispaa ya Bukoba yamegusia viashiria na vyanzo vya uvunjifu wa amani ikiwemo ya malezi katika familia, kutokusimamia vyema misingi ya utawala bora katika jamii, upotoshwaji wa haki za binadamu matumizi mabaya ya lugha na mapungufu katika utoaji mafunzo.

Wakifafanua vizuri darasani wakufunzi ambao ni Msabila Raphael, Justin Hassan Jackson wamesema mafunzo hayo yamelenga kuwaandaa vyema mabalozi wa amani ili waweze kufanya kazi hiyo kwa weledi wanapopeleka elimu hiyo kwa jamii.
Vipengele hivyo vyenye viashiria vya uvunjifu wa amani vimeyagusia maeneo mengi ikiwemo ya malezi katika familia ambapo mkufunzi Msabila ametolea mfano hali ili kwa sasa katika kushuka kwa kiwango cha maadili kwenye jamii na changamoto zake kuanzia ngazi ya familia na kuendelea.
Kwa ujumla wanadarasa wameyajadili mengi kulingana na malengo ya taasisi kama ambavyo mkurugenzi wa taasisi Maulid Rashidi na makamu mkurugenzi Mchungaji Venant Clavery walivyoeleza kuwa maadili yanayotakiwa ni ya kiroho na elimu kwa vitendo.

Naye mkufunzi Justin Hassan Jackson amewasisitiza wanataasisi wawapo majukwaani na maeneo mengine kuzingatia vipengele vya uvunjifu wa amani kama walivyojifunza kwania ya kusaidia kuvithibiti mapema.